Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko TLS yatakiwa kuwajengea uwezo wanacha wake
Habari Mchanganyiko

TLS yatakiwa kuwajengea uwezo wanacha wake

Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Boniphace Luhende
Spread the love

 

WAKILI Mkuu wa Serikali amekitaka Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) kuendelea kuwajengea uwezo wanachama wake ili waweze kufanya kazi kwa weledi na kushirikiana miongoni mwao hasa katika kazi zinazohitaji wabobezi wa maeneo mahususi ya sheria. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yameelezwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Boniphace Luhende akiwa ofisini kwake leo alipokutana na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chama cha Mawakili Tanganyika aliyefika kwa ajili ya kujitambulisha.

Amesema kuwa changamoto iliyopo kwa sasa ni kuwa Mawakili wachache sana wamejikita katika eneo moja la ubobezi. Jambo hili linawanyima Mawakili fursa ya kushiriki katika miradi ya kimkakati iliyopo hapa nchini kwa sasa.

Dk. Luhende amesema kuwa anafahamu namna TLS inavyoshirikiana na taasisi za Serikali na kuipongeza Menejimenti ya TLS kwa kufanya kazi vizuri na kwa kutambua kuwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ni wadau wa TLS.

‘‘Mdau mkubwa wa TLS ni Serikali kwa sababu ndio muajiri mkubwa na wanachama wengi wa TLS wanatoka hapo na ndio ina watu wengi na miradi mikubwa hivyo huwezi kuikwepa Serikali,“ amesisitiza Dk. Luhende.

Amewataka TLS kufanya utafiti kwenye mada wanazozitoa kwenye semina mbalimbali ili ziendane na mahitaji ya wanachama wao ili waajiri waone umuhimu wa kuwapeleka Mawakili kuhudhuria semina hizo.

Dk. Luhende amesema kuwa TLS wana jukumu la kuhakikisha kwamba Mawakili wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili, weledi na miiko ya taaluma yao ili kuitendea haki sekta ya sheria nchini na wadau wanaowahudumia.

Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa TLS, Mariam Othman ameiomba Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kuendeleza ushirikiano uliopo kwa kuendelea kuwafanya Mawakili wa Serikali wanachama hai wa TLS na kuendelea kushiriki katika chama hicho.

“Tumeona ni vema kufika kuonana na wewe ili tujitambulishe na kuomba ushirikiano huo kwa kuwa Mawakili wengi ni wanachama wa TLS,“ amesema Othman.

Pia, Othman ameomba Mawakili wa TLS ambao sio waajiriwa Serikali kupewa nafasi ya kuteuliwa kuwa wasuluhishi katika mashauri ya usuluhishi yanayohusisha taasisi za umma.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Udhibiti Ubora na Menejimenti ya Kesi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mercy Kyamba ameishukuru TLS kwa kuendelea kufanya kazi kwa vitendo na kudumisha ushirikiano na Ofisi hizi mbili na kuwaomba kuangalia jinsi ya kuwafutia Mawakili wa Serikali ambao ni wanachama wa TLS malimbikizo ya ada za uanachama.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Mashauri ya Madai ya Ndani wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, ndugu Deodatus Nyoni amesema kuwa TLS iweke utaratibu wa kuwapatia cheti cha uzoefu cha uendeshaji wa mashauri Mawakili wa Serikali wanaohudhuria mafunzo yanayoendeshwa na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali. Pia alishauri TLS kutambua Mawakili wanaoendesha mashauri kwenye Mahakama za Rufaa kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Sarah Mwaipopo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

Habari Mchanganyiko

Yara yaja na bima ya mazao kwa wakulima

Spread the love  WAKATI serikali ikiweka mikakati mbalimbali kuimarisha sekta ya kilimo...

error: Content is protected !!