Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa TLS yagonga nyundo mbele ya JPM
Habari za SiasaTangulizi

TLS yagonga nyundo mbele ya JPM

Spread the love

MFUMO wa sheria za jinai ulioko sasa nchini, hauna tofauti na sheria za kikoloni, zilizotumika kutia hofu wananchi ili watii amri za kikoloni bila kuhoji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Dk. Rugemeleza Nshala, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), leo tarehe 6 Februari 2020, jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini.

Dk. Nshala ameishuri serikali ya Rais John Magufuli kufanya mabadiliko ya sheria katika mfumo huo, ili kuondoa sheria kandamizi zinazonyima watuhumiwa dhamana.

“Niongelee mabadiliko ya sheria katika mfumo wa jinai na haswa pale mambo makubwa yanayohusu mihili yetu, mfumo wetu wa jinai kubaki na msingi ya kikoloni, ambayo malengo yake yalikuwa kushikilia mtumwa katika kipindi kirefu ndani ya mahabusu au magereza kwa lengo la kutia hofu wananchi ili watii amri za kikoloni bila kuhoji,” amesema Dk. Nshala na kuongeza:

“Mfumo wa kikoloni ulivyokuwa, haukuwa na lengo la kumhukumu mtuhumiwa pao kwa hapo, ulikuwa na lengo la kutisha hata sasa waendesha mashtaka hutumia mfumo huo kwa sababu.”

Dk. Nshala amesema, mtuhumiwa kukaa muda mrefu ndani ya mahabusu, kunakwenda kinyume na haki za binadamu, hasa pale mfungwa husika anapobainika kutokuwa na hatia, kwa kuwa hakuna mfumo unaotoa fidia kwa mtuhumiwa aliyekwa ndani kinyume na sheria.

“Ikumbukwe kuwa, muda wa mwanadamu hapa dunia una ukomo, na hakuna mwenye uwezo wa kuongeza ila Mungu. Kila siku ambayo mtu anapokwa uhuru wake, kwa kuwekwa ndani, siku hiyo haitarudi.

“…na bahati mbaya nchi yetu haina mfumo wa kufidia mtu ambaye alipokwa uhuru wake, na baadaye kesi yake kufutwa au kukutwa hana hatia,” amesema Dk. Nshala.

Kiongozi huyo wa TLS amelishauri Jeshi la Polisi pamoja na Ofisi ya Waendesha Mashtaka, kukamata mtuhumiwa pindi wanapokamilisha upelelezi, sambamba na kuheshimu haki ya mtuhumiwa kupata dhamana.

“Inabidi polisi na waendesha mashtaka wahakikishe wanapotoa amri ya kumkamata mtu, upelelzi uwe umekamilika. Haki ya kupata dhamana iheshimike, hadi sasa watuhumiwa wengi wako ndani licha ya makosa yao kudhaminiwa kisa kuwekewa hati ya mwanasheria mkuu ya kuzuia dhamana,” amesema.

Wakati huo huo, Dk. ameikumbusha serikali na wananchi, kwamba Tanzania ni nchi ya Jamhuri, hivyo inapaswa kuheshimu misingi ya Katiba na Sheria za Nchi.

 “Ni adhimisho muhimu ambalo linatukumbusha juu ya msingi mkuu wa utawla wa nchi yetu. Tunakumbushwa na kusisitizwa kwamba, nchi yetu ni ya kijamhuri na kisemokrasia ambayo inaongozwa kwa katiba na sheria,” amesema Dk. Nshala.

Amesema, hakuna mtu aliyepewa kinga ya kutofuata misingi hiyo, na kwamba anayekiuka anatakiwa kuwajibishwa.

“Kwamba wote wako chini ya sheria na wanatakiwa kuheshimu Katiba na Sheria, hakuna hata mmoja aliyepewa kinga ya kutofuata Katiba na Sheria. Na anayekiuka anatakiwa kuwajibishwa na sheria kwa taratibu za kisheria.

“Tunapozungumzia utawala wa sheria, hatuzungumzii utiifu wa sheria kandamizi. Watu wanatakiwa kukosoa utungwaji wa sheria zinazopoka na haki zao za msingi, amabazo zinalindwa na msingi wa Katiba yetu na hata kupinga sheria hizo mahakamani,” amesema Dk. Nshala.

Akizungumzia juu ya utendaji wa mhimili wa mahakama, Dk. Nshala ameshauri wananchi na viongozi wa umma kuheshimu uamuzi unaotolewa na mhimili huo, hata kama hauwapendezi.

“Tunakumbushwa majukumu muhimu ya mhimili wa mahakama, huu ndio wenye jukumu azizi la kutoa haki kwa tafisri sahihi wa katiba na  sheria.

“Kwa lugha ya kisheria, mahakama ndio mlinzi asiyeyumba wa Katiba na utawala sheria, pale mahakama inapotoa uamuzi wake, wanatakiwa kuheshimu na kutekeleza uamuzi huo hata kama haupendi paispo kuathiri haki ya wadaiwa ya kukata rufani au kuomba marejeo,” amesema Dk. Nshala.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

error: Content is protected !!