CHAMA cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), limeendesha kongamano la wazi la kukusanya maoni ya wadau juu ya namna ya kuboresha taasisi ya haki jinai nchini. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Kongamano Hilo limefanyika leo tarehe 11 Machi 2023, katika makao makuu ya TLS, jijini Dar es Salaam na kuongozwa na aliyekuwa Rais wa chama hicho, Fatma Karume.
Akifungua kongamano hilo, Makamu Mwenyekiti wa TLS, Gloria Kalabamu amesema maoni yatakayokusanywa yatapelekwa katika kikosi kazi kilichoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan, kuangalia namna ya kuboresha mfumo na taasisi za haki jinai.
“Hivi karibuni Dk. Samja ameunda tume kuangalia namna ya kuboresha taasisi haki jinai nchini, imeabza kazi na inakusanya maoni kwa sasa ambayo yatawezesha maboresho ya taasiai ya haki jinai,” amesema Kalabamu na kuongeza:
“TLS kama mdau wa sheria tumekuwa tukifanya makongamano mbalimbali kwa ajili ya kukusanya maoni kusudi tupate maoni ya watu mbalimbali, tumeona ni vyema wadau muhimu tukakusanyika tuangalie namna ya kushauri Serikali kufanya mfumo wa haki jinai inakuwa bora.”
Mbali na Karume, waongoza mdahalo huo ni Wakili Mwandamizi, Mpare Mpoki na aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Beatus Malima.
Leave a comment