Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Biashara TLS wajitosa sakata la ukodishaji wa bandari
BiasharaTangulizi

TLS wajitosa sakata la ukodishaji wa bandari

Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Harold Sungusia
Spread the love

 

CHAMA cha wanasheria Tanzania (TLS), kimejitosa katika sakata la umilikishwaji wa bandari baada ya serikali kuanzisha makubaliano ya awali na kampuni ya kigeni ya DP World, kutoka Falme za Kiarabu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hatua ya TLS – Tanganyika Law Society (TLS) – kimejitosa katika sakata hilo, kufuatia kuibuka kwa mjadala kuhusiana na mazingira ya makubaliano hayo wakihofia huenda nchi  ikabanwa katika siku za usoni.

Mjadala kuhusu suala hilo, umatarajiwa kufikishwa bungeni, kesho Jumamosi, tarehe 10 Juni 2023.

Bunge la Jamhuri, ndicho chombo kilichokabadhiwa dhima ya kupitisha makubaliano hayo yatakayofahamika kama Azimio la Bunge kuhusu uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari Tanzania.

Katika taarifa yake kwa umma, TLS kimeeleza jinsi kinavyoendelea kuufuatilia mjadala huo ambao kiini chake, ni makubaliano yanayoipatia Serikali ya Dubai, mamlaka ya uendeshaji na usimamizi wa bandari zote Tanzania Bara, ikiwamo bandari kongwe ya Dar es Salaam.

Bandari ya Dar es Salaam, ni ndiyo bandari kuu, inayaunganisha mataifa kadhaa ya jirani, ikiwamo Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Malawi, Burundi, Rwanda, Uganda na hata Zimbabwe.

Makamu wa Rais wa TLS, Aisha Sinda amesema, kutokana na unyeti wa suala hilo na namna linavyoendelea kuvuta hisia za wengi, chama hicho kimelazimika kuunda jopo la wataalamu watakaokuwa na jukumu la kuupitia mkataba huo ambao nakala zake zimesambaa kwa umma.

Mkurugenzi TPA, Plasduce Mbossa

Wajumbe wanaounda kamati hiyo ambao ni wanachama wa TLS ni wataalamu wa masuala ya sheria za mikataba ambao pamoja na mambo mengine, watakuwa na kazi ya kupitia na kufanya uchambuzi wa kisheria juu ya makubaliano hayo.

Kamati hiyo iliyoundwa na Rais wa TLS, Harold Sungusia, haijaelezwa ni lini inaanza kazi yake, ingawa imesalia na siku nne kuanzia leo kabla ya kuwasilisha ripoti yake kwa Baraza la Uongozi.

Wengi wanasubiri kuona namna Bunge hilo litakavyolijadili jambo hilo, ingawa wakati mmoja kulijitokeza sura ya mgawanyiko miongoni mwa wabunge hao wakati walipokuwa wakiijadili bajeti ya wizara ya ujenzi na uchukuzi.

Miongoni mwao waligawanyika; kwa baadhi kutilia shaka namna mkataba huo ulivyoundwa na jinsi kampuni hiyo itakavyopewa idhini ya kusimamia bandari zilizoko nchini.

Lakini wengine waliegemea upande wa serikali wakitoa heko kwa kuorodhesha ufanisi utakaojitokeza wakati ubinafsishaji huo utakapokamilika.

Mapema mwaka jana (28 Februari 2022), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kwa niaba ya serikali, ilijifunga kwenye mkataba wa awali (Memorandum of Understanding- MoU) na kampuni ya DP World (DPW) ya Dubai.

Mkataba huo wa awali umetaja maeneo ambayo DPW inakabidhiwa, ni pamoja na bandari zote za bahari na maziwa makuu, maeneo maalum ya kiuchumi (special economic zones), maeneo ya maegesho na utunzaji mizigo (logistics parks) na maeneo ya kanda za kibiashara (trade corridors).

Shughuli hizo ni kama pamoja na upembuzi yakinifu, tathmini ya kimazingira na kijamii ya mradi, kujenga barabara za kuwezesha kufika eneo la mradi.

Aidha, pande hizo mbili, zilikubaliana kuwa mchakato wa kuridhia mkataba utaanza ndani ya siku thelathini (30) mara tu baada ya mkataba huo kusainiwa.

Lengo ni kuzibana pande husika za mkataba, kupitia sheria za kimataifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Biashara

Black Gold kasino mgodi wa madini Meridianbet 

Spread the love  Dhahabu ni moja kati ya utajiri wenye thamani kubwa...

error: Content is protected !!