Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko TLS, wagombea urais wavutana
Habari MchanganyikoTangulizi

TLS, wagombea urais wavutana

Kaleb Gamaya, Mkurugenzi Mtendaji wa TLS
Spread the love

 

WAKATI baadhi ya wagombea wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), wakijinadi kuthibiti mapato na matumizi  kwenye chama hicho, Kaleb Gamaya ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa chama hicho, amesema hakuna ubadhirifu. Anaripoti Regina Mkonde, Arusha … (endelea).

Amesema, chama hicho kimeweka mifumo madhubuti ya kudhibiti ubahirifu wa mapato na matumizi ya chama hicho tofauti na baadhi ya wagombea wake walivyodai.

Gamaya ametoa kauli hiyo leo Jumatano tarehe 14 Aprili 2021 wakati akizungumza na MwanaHALISI Online, jijini Arusha.

Albert Msando na Flaviana Charles ni miongoni mwa mawakili walioahidi kudhibiti mapato na matumizi ya TLS, ili kuimarisha utendaji wa taasisi hiyo.

Gamaya amesema, TLS ina Kamati ya Bajeti na Ukaguzi ambayo inahakikisha fedha za wanachama zinatumika vizuri.

“Audit and Badget Committe ni ya muhimu sana ili kuhakikisha wanachama fedha zao zinatumika vizuri. Taaluma yetu ni muingiliano, tuna wahasibu, wahandisi na watu wa kila aina,” amesema Gamaya.

Ufafanuzi huo umetolewa kufuatia kauli za baadhi ya wagombea urais wa TLS, katika kampeni zao kusema, watasimamia matumizi ya fedha za chama hicho.

Wagombea hao watano wanaochuana kumrithi Dk. Lugemeleza Nshala anayemaliza muda wake, ni Wakili Flaviana, Dk. Edward Hoseah, Francis Stolla, Shehzada Walli na Msando.

“Kamati hii kwa sababu sababu ni ya fedha imewekwa maalumu kwa watu ambao wamesomea utaalamu wa masuala ya fedha.

Dk. Rugemeleza Nshala, Rais wa TLS

Wako kama tisa, wajumbe saba wote wana CPA na ni wabobezi, ndio maana suala la mashaka ya ufujaji wa fedha halipo. Ni maneno ya juu sababu kamati iliyowekwa, inasimania mifumo,” amesema Gamaya.

Amesema, taarifa kwamba TLS ina matumizi mabaya ya fedha, si sahihi, kwani kamati hiyo huchunguza utekelezwaji wa bajeti msra tatu kwa mwaka.

“TLS ni taasisi, kamati inachunguza na inapendekeza bajeti katika Baraza la Uongozi. Inaangalia mwenendo mzima wa bajeti kila robo ya mwaka. Inajua matumizi ya kila senti ya wanachama,” amesema Gamaya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mchina wa SGR aburuzwa kortini kwa kumjeruhi Mtanzania, TRC waja juu

Spread the love  RAIA wa China, Zheng Yuan Feng, amefikishwa mahakamani kwa...

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

error: Content is protected !!