Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa TLS: Mjadala katiba mpya hauwezi kufa
Habari za Siasa

TLS: Mjadala katiba mpya hauwezi kufa

Dk. Edward Hoseah, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)
Spread the love

 

CHAMA cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), kimemuomba Rais Samia Suluhu Hassan, aunde kamati ya kushughulikia marekebisho ya katiba, ili kutimiza dhumuni la uanzishwaji mchakato wa upatikanaji katiba mpya, uliokwama 2015. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 12 Julai 2021 na Rais wa TSL, Dk. Edward Hoseah, akitoa maoni ya chama hicho kuhusu siku 100 za Rais Samia madarakani, alizozianza tarehe 19 Machi  hadi 27 Juni mwaka huu.

Mchakato huo ulioanza 2011 chini ya Rais wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete, ulikwama 2015 katika hatua ya wananchi kupiga  kura ya kuipitisha rasimu ya katiba pendekezwa, iliyoandaliwa na lililokuwa Bunge la Katiba.

Dk. Hoseah amesema kuwa, suala la upatikanaji katiba mpya haliwezi kufa, kwa kuwa ni takwa la wananchi.

“Jambo hili lipo mikononi mwa rais na sisi tunashauri aunde kamati ndogo ikiwa na watalamu wa kumshauri ili tuweze kuhitimisha hii hatua kubwa, ambayo yeye alikuwa makamu mwenyekiti wa Bunge lililokuwa linashughulikia katiba mpya,” amesema Dk. Hoseah.

Dk. Hoseah ameongeza “mjadala wa katiba mpya hauwezi kufa kwa sababu umo katika mioyo ya Watanzania na Watanzania kuna mambo wanafikiria yanapaswa kutizamwa upya na kurekebishwa vinginevyo tuwe na katiba mpya.”

Dk. Hoseah amemuomba Rais Samia aheshimu maoni ya watu wanaolilia katiba mpya, hata kama ni wachache.

“Sasa hivi kama TLS tunafurahia mjadala unaoendelea una afya,  sababu ni mawazo ya wengi hata kama ya wachache basi mawazo haya yanapaswa kuheshimiwa. Tuna amini hili atalitafakari, tunashuri aunde kamati ndogo tuvuke mto wa vuguvugu hili la katiba mpya,” amesema Dk. Hoseah.

Rais huyo wa TLS ametoa kauli hiyo akizungumzia mjadala wa upatikanaji katiba mpya, uliobuliwa hivi karibuni na baadhi ya vyama vya siasa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s).

“Tunafahamu kuna mjadala unaohusu katiba mpya na sisi TLS tunafurahi wa wananchi wanatoa dukuduku zao, wananchi wanaopoongea ni jambo zuri. Tunamuomba rais alitizame jambo hili maana liko mikononi mwake,” amesema Dk. Hoseah na kuongeza:

“Ni ushauri wetu kwamba kwa jinsi tunavyokwenda akaunda kamati ya kuratibu hapa tulipofika, aidha kuwa na katiba mpya au kuboresha iliyopo iweze kukidhi karne ya 21.”

Mchakato wa upatikanaji katiba mpya, ulikwama kutokana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kutokamilisha daftari la wapiga kura.

1 Comment

  • Asante ndugu Edward wananchi hawana fikra za katiba mpya wananchi wanaelewa kwamba katiba sio maendeleo ya nchi wanacho hitaji ni huduma za jamii zikamilike na ziwe za uhakika sasa unavyo endeleaza na kulikumbusha swala la katiba mpya wananchi hawakuelewi bora hata ungeleza serekari iongeze vitendea kazi katika kikosi cha zima moto

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!