Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Tito Magoti afungua kesi akitaka fidia kutopiga kura uchaguzi 2020
Habari Mchanganyiko

Tito Magoti afungua kesi akitaka fidia kutopiga kura uchaguzi 2020

Wakili Tito Magoti, Mtumishi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
Spread the love

 

MTETEZI wa haki za binadamu, Tito Magoti ameifikisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, akiitaka imlipe fidia kwa kushindwa kumwekea mazingira ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, akiwa mahabusu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online kwa simu, leo tarehe 2 Machi 2022, Tito amedai mbali na NEC, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya kikatiba namba 3/2022, ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Jeshi la Magereza.

“Nimefungua kesi ya kikatiba, Mahakama Kuu, dhidi ya NEC, AG, CHRAGG na Magereza, kuomba Mahakama ifute sheria inayozuia wafungwa kupiga kura,” amesema Tito.

Tito amesema “aidha, ninaiomba mahakama itoe tamko la kutotimiza wajibu na amri ya kunilipa fidia dhidi ya NEC na wenzake. Ni kwa uzembe wao mimi na maelfu ya mahabusu hatukuwekewa mazingira ya kupiga kura 2020, japo hakuna sheria iliyotuzuia.”

Mbali na maombi hayo, Tito amedai yeye na mwezake, John Tulla, wanaiomba mahakama hiyo ilinde haki ya wafungwa na mahabusu kushiriki uchaguzi.

Amesema kesi hiyo itatajwa mbele ya Jaji John Mgetta, tarehe 7 Machi mwaka huu, ambapo atawakilishwa na Wakili John Seka.

“Kesi itatajwa tarehe 7 Machi 2022, mbele ya Jaji Mgetta, J. Mimi na John Tulla tunaiomba Mahakama ilinde haki ya wafungwa na mahabusu kushiriki uchaguzi, hususan kupiga kura. Tunawakilishwa na Wakili John Seka,” amesema Tito.

Tito na mwenzake, Theodory Giyan, walikamatwa mwezi Desemba 2019, wakituhumiwa kwa makosa ya kupanga kumiliki program za kompyuta, iliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya kufanya uhalifu na kupelekea kujipatia Sh. 17,354,535.

Tito na Giyani walisota rumande kwa takribani mwaka mmoja, hadi walipoachwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, baada ya kulipa fidia ya Sh. 17.3 milioni.

Wlilipa fedha hizo baada ya kukiri makosa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

error: Content is protected !!