September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tishio la corona: Ibada KKKT, Misikiti zabadilishwa mwelekeo

Spread the love

WAKATI baadhi ya misikiti ikitumia dakika 20 pekee katika Ibada ya Ijumaa, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) sasa litaumia dakika 45 pekee kwenye ibada zake za Jumapili. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Waraka wa kanisa hilo uliotiwa saini na Mkuu wa Kanisa hilo, Askofu Fredrick Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ya KKKT, umesambazwa na kusomwa leo tarehe 5 Aprili 2020 kwenye makanisa hayo.

Kwenye waraka huo, hatua hiyo imefikiwa kutokana na tishio la dunia la kusambaa kwa virusi vya corona (COVID-19), na kwamba hatua hiyo inalenga kupunguza kusambaa kwa virusi hivyo.

Hatua ya KKKT imetanguliwa na baadhi ya misikini kupunguza muda wake wa ibada ya Ijumaa, kutoka dakika 50 mpaka dakika 20.

Miongoni mwa misikiti iliyopunguza muda wa ibada ni pamoja na Msikiti wa Answaar, uliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Katika agizo hilo kwa KKKT, dayosisi zote nchini Askofu Shoo amesema, makanisa hayo yalikuwa yakitumia saa moja na nusu, lakini sasa watatumia dakika 45 tu huku akitoa wito kwa kukaa urefu wa mira mbili kutoka muumini mmoja kwenda mwingine.

Amesema, uamuzi huo ni maagizo ya Halmashauri Kuu ya Dayosisi na kwamba, kwa wamauni wataoshindwa kufika kanisani kwa ajili ya ibada, watatuma sadaka zao kupitia miamala ya simu.

error: Content is protected !!