August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tisa wafariki katika mlipuko wa bomu Somalia

Spread the love

 

WATU tisa wamefariki dunia huku wengine kadhaa wakijeruhiwa, katika mlipo wa bomu la kujitoa muhanga, uliotokea kwenye Mji wa Marka, nchini Somalia. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Miongoni mwa waliofariki dunia ni Mkuu wa Wilaya, Abdullahi Wafow na baadhi ya walinzi wake.

Aidha, kundi la wanamgambo wenye itikadi kali la Al-Shabaab, limekiri kuhusika katika tukio hilo.

Hili ni miongoni mwa matukio ya kujitoa muhanga, yaliyopoteza maisha ya watu nchini Somalia ambapo lingine lilitokea katika Mji Mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu na kuua watu tisa

error: Content is protected !!