January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Timu ya Makipa yaichapa 3-0 Taswa FC

Wachezaji wa timu ya Taswa FC wakiwa makini kuzuia shambulio la timu ya Makipa

Spread the love

Timu ya soka ya Chama Cha Magolikipa Tanzania (TAGA) imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Timu ya soka ya waandishi wa habari za Michezo nchini (Taswa FC) katika mchezo maalum wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Bora, Kijitonyama jijini.

Mchezo huo maalum awali ulitakiwa kufanyika kwenye uwanja wa Karume,  ulihamishiwa uwanja wa bora kutokana na ‘Mizengwe’ ya dakika za mwisho  ya wamiliki wa uwanja huo.

Timu zote zilianza mchezo huo kwa kasi na kukosa nafasi kadhaa za wazi. TAGA ndio ilikuwa ya kwanza kulifikia lango la Taswa FC ambayo ilizindua jezi zake kwa mara ya kwanza zilizotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB), hata hivyo mshambuliaji wake, Ivo Mapunda akipiga nje.

Makipa walikuwa katika nafasi nzuri ya kufunga tena katika dakika ya sita ya mchezo, hata hivyo penalti ya Shaaban Kado ikipanguliwa na kipa wa Taswa, Ahmed Famau.

Taswa FC iliibuka katika dakika ya nane ya mchezo na Zahoro Mlanzi alikosa bao la wazi akiwa na kipa wa TAGA FC, Fatuma Omari ambaye pia alifanya kazi ya ziada kuokoa mipira miwili ya kona iliyokuwa ikiingia wavuni kutoka kwa Majuto Omary.

Pamoja na kuwa na umri mkubwa na kutofanya mazoezi kila siku kulinganisha na timu ya makipa, wachezaji wa Taswa, Ali Mkongwe, Martin, Majuto, Ibrahim Masoud,  Zahoro Mlanzi, Shafii Dauda, Wilbert Molandi, Sweetbert Lukonge, Muhidini Sufiani, Salum Jaba, Juma Ramadhani na Julius Kihampa walionyesha uwezo mkubwa katika mchezo huo .

 Makipa walitumia mazoezi yao ya kila siku vizuri na kupata bao katika dakika ya 14 lilolofungwa na Mapunda kufuatia krosi safi ya Saleh Malande alicheza vizuri na Juma Kaseja na Ali “Barthez” Mustapha ambaye pia alifunga bao la tatu. Bao la pili la makipa lilifungwa na Shaaban Kado baada ya kazi nzuri ya Deogratius “Dida” Munishi.

Rais wa makipa hao, Alex Ndembeka alisema kuwa wamefarijika sana mchezo huo ambao umetumika rasmi kuzindua chama chao ambacho lengo lake kubwa ni kuendeleza fani hiyo kwa kuvumbua vipaji na kuondoa fikra za kuwa ‘magolikipa’ hawapendani.

“Tunawapongeza waandishi kwa kukubali wito wetu na kufanikisha kuzindua chama hiki, nadhani umeona jinsi ilivyo kwa makipa wetu kucheza pamoja, kufurahi na kuondoa mtazamo hasi wa kuwa makipa hawapendani,” alisema Ndembeka.

error: Content is protected !!