July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Timbwili uchaguzi Meya Dar es Salaam

Spread the love

UCHAGUZI wa Meya wa Jijini la Dar es Salaam umegeuka kitendawili baada ya Kaimu Mkurugenzi wa Jiji kuahirisha kwa mara ya nne, anaandika Happyness Lidwino.

Kumekuwepo na sintofahamu ya kupatikana kwa Meya wa Jiji kutokana na mvutano uliopo kati ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam ulipangwa kufanyika leo lakini kutokana na kuendelea kwa mvutano kuhusu washiriki walio na sifa ya kushiriki upigaji kura kwenye uchaguzi huo kutopatiwa ufumbuzi, mgogoro huo umeendelea kutokea.

Taarifa zaidi kuhusu kinachoendelea zitakujia hivi punde.

error: Content is protected !!