Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Mapadri 25, Masista 60 waaga dunia Tanzania
Habari MchanganyikoTangulizi

Mapadri 25, Masista 60 waaga dunia Tanzania

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tazania (TEC), Padri Charles Kitima
Spread the love

 

TAKRIBANI mapadri 25, masista, manesi na madaktari 60 wa Kanisa Katoliki Tanzania, wamefariki dunia kutokana na tatizo la kupumua, ndani ya kipindi cha miezi miwili iliyopita. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

“Ndani ya siku 60, tumepoteza mapadri zaidi ya 25 na masista na manesi 60 wa kanisa letu,” ameeleza Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dk. Charles Kitima.

Dk. Kitima ametoa kauli hiyo, leo Jumatano, tarehe 3 Machi 2021, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam.

Alikuwa akitoa tathimini ya maambukizi ya virusi vya Corona, vinavyosababisha kuwapo kwa tatizo la kupumua.

Amesema, “mpaka sasa, kwa miezi miwili hii, kuna mapdri zaidi ya mapadri 25 wamefariki kwa tatizo la kupumua. Hili halijapata kutokea; tulizoea mapdari watatu au wanne kwa uzee na mengine.”

Aliongeza, wengine waliofariki dunia katika kipindi hicho, ni masisita, manesi; na au madaktari. Ametaja jumla yao kuwa ni zaidi ya 60.

“Vifo vinaendelea na hivyo, muhimu tuchukue tahadhari. Tufike wakati tuchukue tahadhari, Corona ipo, tusifanye mzaha katika hili,” amesisitiza Padri Kitima.

Amesema, wao kama kanisa, hawafahamu vifo vinavyotokea kwa sasa kama ni corona au la, lakini “kwa sasa tunaambiwa watu wanafariki kwa tatizo la kupumua.”

Kiongozi huyo wa kiroho amesema, kwa sasa kila Mtanzania anahitaji kuchukua tahadhari kujikinga na magonjwa mbalimbali ikiwamo Corona, na hilo la kupumua kwa kunawa mikono, kuvaa barakoa na kutokukaa karibu.

Padre wa Parokia ya Kristo Mfalme Kibaoni, Jimbo Katoliki la Singida, Marehemu Parick Njiku

TEC imetoa wito kwa waumini wake na wananchi kwa ujumla, kuchukua tahadhari, na kwamba serikali ina wajibu wa kutoa taarifa sahihi kuhusu ugonjwa huo wa Corona.

Kupatikana kwa taarifa kuwa mapadri 25, masista na manesi 60 wamefariki dunia nchini, kumekuja takribani mwezi mmoja, tangu kanisa hilo, kutahadharisha kuwapo kwa tishio la virusi vya corona nchini.

Katika tamko lake, TEC ilisema, ni muhimu kwa wananchi kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona na ugonjwa wa uviko (COVID-19).

Andishi la kanisa hilo, lilitumwa kwa Mwadhama, Mpelekwa wa Baba Mtakatifu, Maaskofu Wakuu, Maaskofu na Maaskofu Wastaafu. Lilisainiwa na Rais wa TEC, Askofu mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Mbeya, Gervas Nyaisonga.

TEC walifika mbali zaidi kwa kueleza kuwa kumeibuka wimbi jipya la maambukizo ya Corona ulimwenguni na kwamba “nchi yetu siyo kisiwa.”

Naye Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Isaac Aman, alieleza kuwa Mungu hajaribiwi. Ametaka wananchi kujikinga na maambukizi ya Corona.

Askofu Amani alisema, “…tusimjaribu Mungu kwa kufanya uzembe na maisha yetu. Turejee tahadhari za kuzuia maambukizi bila ya kuwa na hofu.

Marehemu Padri Ernest Donald Boyo, aliyekuwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Chang’ombe

Katika waraka huo aliyoupa kichwa cha maneno kisemacho, “Kutembea Pekupeku Juu ya Mbigili,”Askofu Amani alisema, watu wanapaswa kuendelea kuchukua tahadhari kwa kuwa ugonjwa huo upo na unatesa mataifa mengi duniani.

Alisema, “maji ya kunawa kanisani yameondolewa, na pengine yapo lakini watu hawanawi tena kwa imani kwamba hakuna Korona. Hata ile tahadhari ya kutoshikana mikono watu wamejiondolea wenyewe kwa imani kwamba, hakuna Corona.”

Akizungumza kwa ukali iliyosheheni ucha Mungu, Padri Kitima amesema, ni wakati sasa kwa wanasayansi Tanzania, kufanya utafiti kinachosababisha mamia ya watu kufariki dunia katika kipindi kifupi kama hicho.

Amesema, nchi zingine duniani zinakwenda haraka na wamepunguza tatizo, lakini tangu mwaka jana, wanasayansi nchini Tanzania, hawajafanya utafiti wowote.

“Mfano sisi Kanisa Katoliki tuna hospitali na vituo vya afya zaidi ya 500, lakini haturuhusiwi kupima Corona kwa sababu hatuna vifaa.

“Lakini watu wanakufa tunaambiwa tatizo la kupumua, nimonia. Sasa sisi kama taasisi tunaongoza kwa ukweli kama Injili ya Yohana 8:32 inasema ukweli itawapeni uhuru.”

Padri Dk. Kitima anasema, “wanatuambia kwamba ukimweleza mtu kuwa ana tatizo hilo, utamjaza hofu. Hapana. Magonjwa haya hayajaanza leo, tunapaswa kujenga ukweli, na ukweli unapatikana kwa njia ya tafiti.”

Akizungumza kwa uchungu, Katibu mkuu huyo wa TEC anasema, “hii dhana kwamba ugonjwa umeondoka, haipo…tuwe makini na huu ugonjwa na tahadhari ichukuliwe. Sisi hatutasitisha huduma ila tujengewe uwepo wa kufikiri kwa kupewa taarifa sahihi.”

Katika maelezo yake, Padri Kitima amesema, mbali na kumwomba Mungu, lakini hatua za tahadhari zinapaswa kuzingatiwa na kila mmoja.

“Huyu Mungu si hirizi, anataka kila binadamu awajibike na atumie uwezo wake kufikiri. Corona ipo, unaambiwa chukua tahadhari, unasema mimi nasali. Mungu wetu anataka watu wawajibike, si kusema tu, tunasali,” amesisitiza Padri Kitima.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, Milioni 180…

Spread the loveMSIMU wa tatu wa Kampeni ya kuhamasisha utamaduni wa Kuweka...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

error: Content is protected !!