May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tiketi elfu 11 zimeshauzwa mchezo Simba na Yanga

Spread the love

 

JUMLA ya tiketi elfu 11 zimeshauzwa kuelekea mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho (FA) kati ya Simba dhidi ya Yanga utakaopigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Kigoma … (endelea).

Mchezo huo utapigwa siku ya Jumapili, tarehe 25 Julai 2021, kuanzia majira saa 10 jioni.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, mkoani Kigoma, Meneja Biashara wa kampuni ya N-Card ambao wakatishaji tiketi kwenye mchezo huo wa fainali, Jackson Jaka amesema kuwa mpaka sasa zoezi hilo linaenda vizuri bila changamoto yoyote.

“Zoezi linaendelea vizuri hakuna tatizo lolote lilojitokeza mpaka sasa na huduma bado zinaendelea,” alisema Meneja huyo.

Meneja huyo aliongezea kuwa wameweka vituo 11 kwa ajili ya kufanya mauzo hayo kwenye mji wa Kigoma, huku kati ya vituo hivyo, saba ni magari yanayotembea maeneo mbalimbali na vituo vinne ni rasmi.

error: Content is protected !!