June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tigo yawapiga tafu CCBRT kutibia watoto walemavu

Watoto wenye ulemavu wa miguu wakikabidhiwa msaada wa baiskeli

Spread the love

KAMPUNI ya Tigo Tanzania, imetoa msaada wa Sh. 320 million, kwa hospitali ya CCBRT ikiwa ni sehemu ya mchango wa kugharamia matibabu ya watoto wanaozaliwa na ulemavu wa miguu. Anaandika Sarafina Lidwino … (endekea).

Akizungumza katika tukio hilo, lililofanyika katika viwanja vya CCBRT Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez amesema, mchango huo walioutoa leo ni kielelezo tosha kwamba Tigo wanamchango mkubwa katika sekta ya afya nchini.

Amedai, Tigo imekuwa na kawaida ya kutoa michango mbalimbali katika jamii, kwani hata miaka mitatu iliyopita walichangia watoto wenye ulemavu wa midomo.

“Mchango ule uliwanufaisha watoto zaidi ya 1,300, ambao walikuwa wakizaliwa na matatizo ya midomo, kwa miaka mitatu iliyopita.

“Huu ni ufanisi wa kujivunia, kwetu sisi na kwa wenzetu wa CCBRT, ambapo kwa pamoja tumefanikiwa kuleta mageuzi makubwa katika maisha ya watoto hawa na familia zao,” amesema Gutierrez.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa CCBRT, Erwin Telemans, amesema, zaidi ya watoto 1,700 nchini huzaliwa na ulemavu wa miguu.

Ameendelea kusema: “Watu wenye ulemavu wa miguu, hupata ugumu wa kuhudhulia katika shughuri mbalimbali za kimaendeleo, ikiwemo shule.”

Aidha, Talemans amewashukuru tigo kwa msaada waliopeleka na kusema: “Jambo hili linaweza kuepukika mapema endapo watoto watapata matibabu wakiwa na umri mdogo. Hivyo nitoe wito kwa wazazi wote wawapeleke watoto wao hospitali haraka zaidi, pindi wakigundua mtoto ana ulemavu.”

error: Content is protected !!