January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tigo yapiga ‘tafu’ wanahabari

Spread the love

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Tigo imekabidhi vifaa mbalimbali vya michezo pamoja na fedha vikiwa na thamani ya Sh. 8,000,000 kwa Chama cha Waandishi wa Habari Dodoma (CPC). Anaandika Dany Tibason.

Akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo, meneja mawasiliano wa kampuni hiyo, John Wanyancha amesema, wametoa vifaa na fedha kwa waandishi wa habari kwa ajili ya kufanikisha sherehe za bonanza la kufunga mwaka 2015 na kufungua mwaka 2016.

Amesema kampuni inatambua kuwa, waandishi ni kada muhimu kwa jamii na hilo linatokana na kwamba, waandishi wa Mkoa wa Dodoma wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na jamii pia kampuni hiyo.

“Tumeamua kutoa vifaa hivi kwenu waandishi wa habari ili muweze kufanikisha bonanza, ninyi ni chachu na nguzo ya maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla,” amesema Wanyancha.

Amesema, wametoa vifaa hivyo kwa kuwa pamoja na kufanya shughuli za kimitandao lakini pia wanashiriki katika masuala mbalimbali ya kijamii.

Akipokea vifaa hivyo, Mwenyekiti wa CPC mkoani hapo, Habel Chidawali ameishukuru kampuni hiyo kwa kuwasaidia.

Amesema, sherehe hizo za bonanza siyo kwa ajili ya kusherekea tu, bali kutafakari shughuli za tasnia kwa wanachama wa mkoa huo lakini kutafakari zaidi masuala ya kiutendaji mwaka 2016.

“Nia ya bonanza ni kukaa na kutafakari zaidi tumemalizaje mwaka 2015 katika utendaji wetu, lakini pia kutafakari utendaji wetu wa kazi,” amesema Chidawali.

error: Content is protected !!