Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Michezo Tigo, Hisense wapeleka watatu Kombe la Dunia
Michezo

Tigo, Hisense wapeleka watatu Kombe la Dunia

Spread the love

KAMPUNI inayoongoza kwa utoaji wa huduma za kidijitali Tigo Tanzania na Hisense kupitia Promosheni yake ya ‘WAKISHUA TWENZETU QATAR’ na HISENSE wametoa tiketi tatu za kwenda Qatar kushuhudia kombe la Dunia (kwa washindi watatu wa awamu ya kwanza. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Pia Kampuni hizo zimetoa zawadi ya vyombo vya ndani kama vile Friji, Spika za Mziki (SubWoofer), Smart Tv, pamoja na Microwave kwa mshindi mmoja.

Akizungumza leo tarehe 11 Oktoba, 2022 baada ya kukabidhi zawadi hizo kwa washindi Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa, Mary Ruta amesema washindi hao wamepatikana kwenye droo ya kwanza baada ya kufanya miamala mbalimbali ikiwamo kulipa bili.

Pia wamefanya malipo ya kiserikali, kupokea pesa kutoka nchi za nje, benki, mitandao mingine, Lipa kwa Simu, kununua muda wa maongezi  na huduma nyingine mbalimbali za Tigo Pesa.

Alisema baada ya kufanya hivyo waliingia kwenye droo na mwisho wa siku kuibuka washindi wa Kampeni hiyo ya WAKISHUA TWENZETU QATAR NA HISENSE,.

“Tunawasihi wateja wetu endeleeni kufanya miamala na Tigo Pesa ili kuibuka mshindi maana tiketi na zawadi bado zipo

Promosheni yetu ndo kama inaanza maana tutahitaji kupata washindi 50 watakaojishindia safari ya kwenda kuangalia mechi za Kombe la Dunia pamoja na washindi 30 watakaojishindia vifaa vya nyumbani ” alimalizia.

Kwa upande wake Ofisa Masoko wa Kampuni ya HISENSE, Joseph Mavura amesema kuwa kampuni hiyo inatoa ofa ya punguzo la asilimia 20 katika maduka yao yote kwa mteja atakayenunua bidhaaa na kulipia kwa Tigo Pesa.

Naye mshindi wa vifaa vya nyumbani (Friji, Microwave, Smart Tv na Subwoofer) kutoka Hisense,  Jamida Athuman mkazi wa Dar Es Salaam ameipongeza kampuni ya Tigo na Hisense kwa kuja na promosheni hii na kuwasihi watanzania kuichangamkia kwa kufanya miamala mbalimbali na Tigo Pesa huenda wakaibuka washindi kama ilivyotokea kwake ”

Aidha, mmoja ya washindi wa Safari ya kwenda Qatar, Wilson Masawe amesema kuwa ” Ninayo furaha sana kuibuka mshindi wa kwenda Qatar kutazama kombe la dunia kwa mwaka huu 2022 , hakika nimefurahi sana maaana sikutegemea.

Alisema kwa mara ya kwanza maishani mwake anapata nafasi ya kwenda kuitazama timu yake ya Brazil.

“Nawaahukuru sana Tigo na Hisense kwa fursa hii maana sikutarajia maishani mwangu. Nawasihi watanzania kufanya miamala kwa wingi na Tigo Pesa huenda mkaibuka washindi kama ilivyotokea kwangu maana nafasi bado zipo,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!