May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tiger Wood apata ajali mbaya, alazwa ICU

Spread the love

 

MCHEZAJI namba moja wa gofu duniani, Tige Wood amenusurika kifo baada ya kupata ajali ya gari Los Angeles, Marekani. Inaripoti Aljazeera … (endelea).

Taarifa zaidi zinaeleza, Wood alipata ajali hiyo asubuhi jana Jumanne tarehe 23 Februari 2021, na kwamba amepata majeraha makubwa hasa ya mguu. Kwa sasa amelazwa hospitali akipatiwa matibabu.

Wood akiwa anaendesha mwenyewe, gari lake liliacha njia na kubilingita mara kadhaa hivyo kuharibika vibaya, chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa.

 

Taarifa za awali zinaeleza, Wood alikuwa katika mwendo mkali kwenye eneo asiloruhusiwa kutembea mwendo huo.

“Alikuwa anajitambua wakati maofisa usalama wakiwa wamefika eneo la tukio,” taarifa ya awali imeeleza hivyo.

error: Content is protected !!