January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tiba Asili wajitetea mauaji ya Albino

Baadhi ya waganga wa kienyeji

Spread the love

SHIRIKISHO la Vyama vya Tiba Asilia Tanzania (SHIVATIATA), limeitaka Serikali ifanye msako wa nyumba kwa nyumba ili kuwabaini wapiga ramli wanaochochea mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), vikongwe na kunajisi watoto kwa imani za ushirikiana. Anaandika Sarafina Lidwino…(endelea).

Mwenyekiti wa shirikisho hilo, Abdulrahman Lutenga, amewaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, wamefanya uchunguzi wa muda mrefu tangu mauaji hayo yalipoanza na kubaini kuna baadhi ya waganga wa kienyeji ambao wamekuwa wakifanya kazi zao kinyume na miiko yao.

Amebainisha kuwa, siku hizi wamezuka waganga wengi ambao hawana usajili wala hawajulikani, ambapo wengi wao wanatoka nje ya nchi kwa ajili ya kuharibu amani iliyopo.

Lutenga amesema, Tiba Asilia zilikuwepo tangu enzi za zamani, na chimbuko la tiba hizi mara nyingi huwa ni za kurithi kutoka kwa wakuu wa ukoo.

Amefafanua kuwa, siku hizi kuna matapeli wengi ambao wamekosa elimu, wana tamaa ya maisha na mila potofu ambazo zinawafanya kutoa masharti magumu kwa wateja wao.

“Nina wasiwasi kwamba, mauaji mengi ya Albino yanafanywa na wapiga ramli wazamiaji, sio wanaotoka ndani ya nchi yetu, kwa sababu mtu haiwezekani atoke Nigeria, Kongo avuke nchi nyingi tu huko aje Tanzania eti awe mganga,”amesema.

Lutenga ameongeza kuwa ramli ni msingi wa Tiba Asili ya Mwafrika, na kwamba inapigwa sehemu nyingi duniani, hivyo wanakataa kuwa ramli sio kipimo cha dawa ya Tiba Asili, ila watumiaji ndio wanaharibu.

error: Content is protected !!