Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko THRDC yawasilisha mapendekezo 500 tume ya Rais Samia, yalilia katiba mpya
Habari Mchanganyiko

THRDC yawasilisha mapendekezo 500 tume ya Rais Samia, yalilia katiba mpya

Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa
Spread the love

 

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umewasilisha mapendekezo yake 500 katika Tume iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan, ili kuangalia namna Bora ya kuboresha mifumo ya haki jinai nchini. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, amesema mapendekezo hayo yamewasilishwa katika tume hiyo Jana tarehe 20 Februari 2023.

Akielezea baadhi ya mapendekezo hayo, Olengurumwa amesema wameshauri marekebisho ya katiba yafanyike Kwa kuwa ndiyo msingi wa Sheria na taasisi zinazosimamia mifumo hiyo.

“Tumependekeza maboresho ya Sheria zote zinazosimamia haki jinai, mfano Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ambayo ndiyo msingi wa mifuno ya utendaji. Lakini taasisi nyingi zimeanzia kwenye katiba kwa hiyo kwa vyoyote vile lazima tutahitaji marekebisho ya katiba ambayo yatatoa majibu ya mapendekezo tuliyowapa tume,” amesema Olengurumwa.

Katika hatua nyingine, Olengurumwa amesema wameshauri makosa yawe na dhamana, hata hivyo jukumu la kutoa au kunyima dhamana lifanywe na mahakama.

Pia, wameshauri kuwe na adhabu za nje ya gereza kwa wanaofanya makosa madogo, ili kuepusha msongamano katika magereza.

Amesema THRDC inapendekeza wafungwa wenye makosa makubwa watenganishwe na wafungwa wenye makosa madogo, huku wakisisitiza magereza yawe shule za mafunzo ili wafungwa wanaporejea uraiani wawe wamestaarabika badala ya kuwa katili.

“Makosa mengi hayana dhamana, mengi Yana vifungo vya kufungwa kukaa ndani badala ya adhabu zile ambazo sio za kukaa ndani. Adhabu za kukaa ndani zinaweza zikachangia uwepo wa watu wengi gerezani,” amesema Olengurumwa.

Mapendekezo mengine yaliyotajwa na Olengurumwa ni, taasisi zinazotoa haki jinai ziache kufanya kazi Kwa kutumia mifumo ya zamani badala yake ziende na wakati kwa kutumia teknolojia.

1 Comment

  • KAMA BADO ANAAMINI “UTI WA MGONGO NI KILIMO” BASI “LIKE FATHER, LIKE SON” HASA KWENYE MAISHA YA “KIFO HAKINA HURUMA” / KIFO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!