Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko THRDC yatinga Kanda ya Ziwa
Habari Mchanganyiko

THRDC yatinga Kanda ya Ziwa

Jiji la Mwanza
Spread the love

 

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umefanya ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, kwa ajili ya kuboresha mikakati ya utoaji huduma za utetezi wa haki za binadamu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo Jumatano, tarehe 11 Agosti 2021, jijini Mwanza, Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, amesema dhumuni la ziara hiyo ni kuangalia maeneo ya kanda hiyo, ambayo hayafikiwi na huduma za utetezi wa haki za wanadamu.

“Ziara hii inalenga kujua maneneo ambayo hayana wadau wa kutosha, kujua maeneo ya kuboresha huduma za mtandao kwa wanachama,” amesema Olengurumwa.

Aidha, Olengurumwa amesema ziara hiyo imelenga kufuatilia utendaji wa wanachama 30 wa THRDC, walioko katika mikoa ya kanda hiyo, Mwanza, Simiyu na Mara.

“Dhumuni kuu la ziara hii kwa wanachama wa mtandao, ni kuweza kuona kazi mbali mbali zinazofanywa na wanachama wa mtandao, maendeleo, mafanikio na changamoto za kiusalama, wanazopitia katika kutetea haki za binadamu katika kanda zao,” amesema OIlengurumwa.

Olengurumwa amesema, THRDC itaendelea kuimarisha huduma zinazotolewa na mtandao huo, ikiwemo utetezi wa haki ya uhuru wa kujieleza, haki za wafugaji, haki za wanawake, haki za watoto, utoaji wa huduma na msaada wa kisheria na utetezi wa haki za kijamii na uwajibikaji.

Huduma nyingine ni, utetezi wa rasilimali, maliasili na haki za kiuchumi, uhuru wa kujieleza na haki za makundi maalum.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Ndege ya Precision Air yaahirisha safari kwa hitilafu, nyingine yatua kwa dharura

Spread the love  NDEGE ya Shirika la Precision Air imeshindwa kufanya safari...

Habari Mchanganyiko

NMB yakabidhi vifaa tiba hospitali Mtwara  

Spread the loveBENKI ya NMB Kanda ya Kusini imetoa msaada wa vifaa...

Habari Mchanganyiko

Kasilda Mgeni anasisitiza umoja, ushirikiano Same 

Spread the love  MKUU mpya wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

error: Content is protected !!