Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko THRDC yataka sheria, sera za maafa zifumuliwe
Habari Mchanganyiko

THRDC yataka sheria, sera za maafa zifumuliwe

Spread the love

 

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umeiomba Serikali ifanye marekebisho katika Sheria na sera zinazosimamia masuala ya majanga ili ziende na wakati. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumamosi, tarehe 7 Agosti 2021 na Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, katika warsha ya kuwajengea uwezo watetezi wa haki za binadamu katika kukabiliana na maafa na majanga, mkoani Dar es Salaam.

“Sera na sheria  za maafa zilizopo zimepitwa na wakati,  ziangaliwe upya mfano kuwe na sheria inayolazimisha kutengwa fedha za kutosha kwa ajili ya kukabiliana na maafa, hasa fidia katika kurejesha mazingira yaliyoharibiwa na maafa hayo,” amesema Olengurumwa.

Olengurumwa amesema kuwa, sera za maafa zilizopo sasa hazishirikishi wadau badala yake zimelekeza jukumu la kukabiliana na maafa kwa Serikali peke yake.

“Na hii ni sababu suala la maafa linaonekana ni la Serikali pekee. Miaka yote magonjwa milipuko imeonekana suala la Serikali pekee. Serikali haiwezi kufika kila mahali, lakini wakati mwingine kosa sio letu sababu sera ya nchi na mifumo haijahamasisha wananchi kuwa sehemu ya majanga,  au elimu haijatolewa kwa wananchi ili wajiandae kukabiliana na maafa,” amesema Olengurumwa.

Mbali na hayo, Olengurumwa ameishauri Serikali na asasi za kiraia zitoe elimu ya kutosha kwa jamii, ya kujikinga na au kudhibiti  na maafa.

“Hivi sasa ukizungumzia maafa watu wanaona ni kuchuliana au kujipangia matatizo. Mtu akiandika wosia anaambiwa anajipangia kufa. Akijiandalia kaburi anasema unajiombe amabaya. Wakati wote maafa yakija tunaumia sana huenda yasitumiize lakini yakija bila kujiandaa yanaleta maafa sana. Inabidi elimu zaidi itolewe,” amesema Olengurumwa.

Akijibu maombi hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Said, amesema sheria zilizopo zinatambua mchango wa asasi za kiraia.

“Tumejipanga vizuri kukabiliana na maafa,  tunashirikiana vizuri na asasi za kiraia katika mustakabali mzima wa kukabiliana na maafa,” amesema Kanali Said.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awalilia 17 waliofariki ajalini wakisafirisha maiti

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wachimbaji wajenga zahanati kuokoa afya za wakazi 2000

Spread the love  ZAIDI wakazi 2,000 wa kijiji cha Nyamishiga Kata ya...

Habari Mchanganyiko

Baada ya Congo DR, Somalia mbioni kujiunga na EAC

Spread the love  TAIFA la Somalia liko mbioni kuwa mwanachama rasmi wa...

error: Content is protected !!