Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko THRDC yapigwa ‘jeki’ ya mamilioni
Habari Mchanganyiko

THRDC yapigwa ‘jeki’ ya mamilioni

Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Kituo cha Watetezi wa Haki za Binadamu Taifa
Spread the love

 

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umepewa fedha Sh. 470 milioni na Shirika la Frontline Defenders la nchini Ireland, kwa ajili ya kuimarisha mikakati ya utekelezaji na ulinzi wa haki za binadamu nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na THRDC, leo Alhamisi tarehe 7 Oktoba 2021, mtandao huo na Shirika la Fronline Defenders, wameingia mkataba huo wa mwaka mmoja, tarehe 5 Oktoba mwaka huu.

“THRDC umesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Euro 180,000, sawa na  Sh. 470 Milioni na Shirika la Frontline Defenders, lililopo nchini Ireland, ili kuimarisha utekelezaji wa mpango mkakati wa taasisi, unaolenga kulinda na kuwaongezea uwezo Watetezi wa Haki za binadamu Tanzania,” imesema taarifa ya THRDC.

THRDC imesema, utekelezwaji wa mkataba huo unaanza Oktoba hadi 2022.

“Makubaliano hayo  yamesainiwa rasmi tarehe 05 Oktoba 2021 na utekelezaji wake utaanza mapema mwezi huu na kumalizika 2022.”

“Fedha hizi zitatumika kuendeleza kazi za taasisi za utoaji mafunzo mbalimbali  kwa watetezi wa haki za binadamu nchini, kuwatetea watetezi wa haki za binadamu hasa wanaopitia changamoto mbalimbali na kuchangia utekelezaji wa sera za taasisi kwa ujumla,” imesema taarifa ya mtandao huo .

Taarifa hiyo imesema, wanufaika wa mradi huu ni watetezi wa haki za binadamu, pamoja na  wadau mbalimbali wa Serikali.

Na kwamba unatarajiwa kuongeza nguvu katika utetezi wa haki za binadamu n  na kuboresha mahusiano kati ya watetezi wa haki za binadamu na taasisi mbalimbali za kiserikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB yafadhili ziara ya mafunzo machinga, bodaboda Dar nchini Rwanda

Spread the loveBENKI ya NMB imefadhili ziara ya siku nne ya mafunzo...

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

Habari Mchanganyiko

Wadau wataka kasi iongezeke marekebisho sheria za habari

Spread the love  WADAU wa tasnia ya habari wametakiwa kuongeza juhudi katika...

Habari Mchanganyiko

TEF yawatuliza wadau wa habari marekebisho vifungu kandamizi

Spread the love  JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limewataka wadau wa habari...

error: Content is protected !!