May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

THRDC yaomba kamati ya kitaifa ya NGO’s

Spread the love

 

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umeiomba Serikali iunde kamati ya kitaifa, kwa ajili ya kuratibu na kutangaza shughuli  za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) na Asasi za Kiraia. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ombi hilo limetolewa leo Ijumaa, tarehe 2 Julai 2021 na Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, katika maadhimisho ya saba ya siku ya watetezi wa haki za binadamu Tanzania, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City mkoani Dar es Salaam.

“Tunaomba iwepo kamati ya kitaifa itakayotazama na kufuatilia mipango ya asasi za kiraia, hasa katika maendeleo ya Taifa. Tunaomba tarifa za Serikali zitaje mchango wa asasi katika taarifa zake kwa umma,” amesema Olengurumwa.

Mratibu huyo wa THRDC, ametoa ombi hilo akisema kuwa, kwa muda mrefu zimekuwa zikifanya kazi za kijamii, lakini mchango wake hauonekani ipasavyo kwa umma.

“Maombi yetu makubwa tunaomba katika taaisis za Serikali kuwe na sekretarieti zinazotambua taarifa za mbalimbali kuhusu asasi za kiraia. Kazi kubwa zinazofanywa na asasi hazionekani kwa umma,” amesema Olengurumwa.

Akitaja mchango wa NGO’s na asasi za kiraia katika maendeleo ya Taifa, Olengurumwa amesema mashirika hayo yanayongoza kwa kuleta miradi ya maendeleo na fedha za kigeni kutoka nje ya nchi kupitia kwa wafadhili.

“Asasi tunaongoza katika uingizaji fedha za kigeni, ni kwa vile hatuna utaratibu mzuri lakini tungekuwa na utaatibu mzuri, mngeona  kundi gani linaloongoza kuleta fedha za kigeni. Ikiwemo sisi tungekuwa wa pili katika kundi linaloongoza kuleta miradi na fedha za kigeni,” amesema Olengurumwa.

error: Content is protected !!