May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

THRDC yampa tuzo ya utetezi wa haki za binadamu Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), wamempa tuzo maalumu Rais Samia Suluhu Hassan, kufuatia mchango wake katika uimarishwaji wa haki za binadamu Tanzania. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia amepewa tuzo hiyo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya THRDC, Jaji Mstaafu, Joaquine Demello, leo Ijumaa, tarehe 13 Mei 2022, jijini Dar es Salaam, katika sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya mtandao huo.

“Tumekupa tuzo hii Rais Samia kwa kuthamini na kutambua kazi kubwa unayofanya unayofanya kwa kuhakikisha watetezi wa haki za binadamu wanafanya kazi na shughuli zao kwa uhakika na wakati pasipo bughuza yoyote,” amesema Jaji Demello.

Naye Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, amesema watetezi wa haki za binadamu wameandaa Makala maalumu kuhusu mchango wa Rais Samia katika uimarishaji haki za binadamu.

“Kazi yako katika eneo la haki za binadamu ni kubwa sana na inaonekana kote Tanzania na duniani, taarifa rasmi kuhusu mchango wako katika kulinda na kueneza haki za binadamu kwa kipindi cha mwaka mmoja imeandaliwa kwa lengo la kutambua na kuweka kumbukumbu kwa mambo uliyofanya,” amesema Olengurumwa.

Makalla hiyo ya video yenye muda wa takribani dakika tano, imeoneshwa kwenye maadhimisho hayo mbele ya Rais Samia.

Katika Makala hiyo, watetezi hao wameonesha masuala mbalimbali yaliyotelekezwa na rais Samia katika kuimarisha haki za binadamu, ikiwemo kuboresha miundombinu ya shule, kurudisha shuleni watoto walioacha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo, kupata mimba wakiwa shuleni.

Mmabo mengine yaliyooneshwa katika Makala hiyo, ni hatua ya Rais Samia kuagiza uimarishwaji utendaji wa vyombo vya utoaji haki ikiwemo mahakama.

Wakati filamu hiyo ikirushwa, watu waliohudhuria sherehe hizo katika ukumbi wa PSSSF Towe, walifurahia na kupiga makofi

error: Content is protected !!