Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko THRDC yalia udukuzi wa taarifa, TCRA yatoa neno
Habari Mchanganyiko

THRDC yalia udukuzi wa taarifa, TCRA yatoa neno

Onesmo Olengulumwa, Mratibu THRDC
Spread the love

 

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umeiomba Serikali nchini humo, kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), iweke sheria zitakazodhibiti uingiliaji wa taarifa za watu kupitia mtandaoni. Anaripoti Regina Mkonde, Morogoro…(endelea).

Wito huo umetolewa na Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, katika mafunzo ya siku tatu ya wanahabari wa mtandaoni iliyofanyika mkoani Morogoro, kuanzia 10 Mei 2021 hadi leo Jumatano.

Olengurumwa ameishauri, TCRA ianzishe sheria ambayo italazimisha mtu kutopewa mawasiliano ya mtu kutoka katika kampuni za mawasiliano, hadi atakapopata kibali cha mahakama.

“TCRA mtusaidie kuimarisha ulinzi wa taarifa za mtandaoni, kuna sheria zipo ila inabidi ziwe tight (bana) yeyote anayetaka kuingilia tarifa za mtandaoni wapate kibali cha mahakama. Katika hili Tanzania tuko nyuma kwenye data protection laws (sheria za kulinda taarifa mtandaoni),” amesema Olengurumwa.

Mratibu huyo wa THRDC amesema, kwa sasa Tanzania inakabiliwa na changamoto ya taarifa na mawasiliano ya watu kuvujishwa huku akitolea mfano sakata la kuvuja kwa mazungumzo ya Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye na wenzake.

“Kampuni za simu zimepokea jumbe za watu wakitaka watoe mazungumzo ya watu, wanaambiwa watoe taarifa za wateja wao. Hii inakiuka haki za binadamu. Mtu akichunguza anatakiwa apate kibali cha mahakamani na kwa sababu maalum, labda za kiusalama wa nchi na kulinda haki za wengine,” amesema Onesmo na kuongeza:

“Mfano mazungumzo ya kina Nape ilitakiwa yabaki kwa wahusika tu kuliko kuyaleta kwa umma, hiyo ni kuingilia privace (faragha) ya mtu.”

Sakata la kuvuja kwa sauti yenye mazungumzo ya Nape na makatibu wakuu wastaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, Yusuf Makamba, wabunge wa CCM, Willium Ngeleja na aliyekuwa mwanachama wa chama hicho kabla ya kufukuzwa, Bernard Membe liliibuka Julai 2019, baada ya kusambazwa mitandaoni.

Mazungumzo hayo, yalihusu utendaji wa aliyekuwa mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli, jinsi anavyoshindwa kukiongoza chama hicho na serikali.

Akijibu maombi hayo, Dk. Philip Filikunjombe, Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi na Utekelezaji wa Sheria wa TCRA amesema, atalifikisha suala hilo katika mamlaka hiyo kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

“Kama taarifa za udukuzi unaendelea watu wanavujisha taarifa za watu, nitalifikisha ofisini kuona kama kuna watu wanafanya vitendo hivyo,” amesema Dk. Filikunjombe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!