July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

THRDC kuzindua mpango mkakati wa maendeleo

Spread the love

 

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), unatarajia kuzindua mpango mkakati wa Asasi za Kiraia (Azaki), wa utekelezaji Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne, tarehe 22 Juni 2021, jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, akizungumza na wanahabari kuhusu maadhimisho ya saba ya siku ya watetezi  wa haki za binadamu Tanzania, yanayotarajiwa kufanyika tarehe 2 Julai mwaka huu.

Olengurumwa amesema, mpango huo utazinduliwa katika maadhimisho hayo, yatakayofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City mkoani Dar es Salaam, huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

“Siku hiyo tutafanya uzinduzi na kukabidhi mpango mkakati wa Azaki wa utekelezaji mpango huo, watetezi wa haki za binadamu wameandaa mpango huo, ambao utatumika kama muongozo kwenye kutambua mchango wa asasi hizo, katika maendeleo ya Taifa  miaka mitano ijayo,” amesema Olengurumwa.

Aidha, Olengurumwa amesema kuelekea maadhimisho ya siku hiyo, THRDC itafanya warsha kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wadau wake,  juu ya namna ya kuzingatia na kuendana na sheria za ulipaji kodi.

Mratibu huyo wa THRDC amesema, mafunzo hayo yataendeshwa na maafisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Shirika la Wajibu ‘Wajibu Institute of Public Accountability’.

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

“Kuelekea maahdimisho THRDC umeandaa baadhi ya warsha mbalimbali zitakazofanyika kabla ya siku hiyo, katika kubadilishana uzoefu na kukuza mahusiano, mafunzo yatakayotolewa ni pamoja na mafunzo juu ya namna ya kuzingatia na kuendana na sheria za ulipaji kodi,” amesema Olenguruimwa.

Olengurumwa ameongeza “tumetengeneza mwongozo utakaoziwezesha asasi za kiraia kutekeleza sheria, kanuni na sera zinazosimamia ulipaji kodi nchini Tanzania.”

Pia, Olengurumwa amesema katika maadhimisho hayo watetezi wa haki za binadamu wataonesha kazi za juu ya utetezi wa haki hizo nchini.

Pamoja na kutoa tuzo kwa watetezi w ahaki z abinadamu pamoja na asasi za kiraia zenye mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa.

 

error: Content is protected !!