July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TGNP yapigania kuondoa vikwazo kwa mwanamke

Spread the love

MTANDAO wa Jinsia (TGNP) umetoa wito kwa serikali na wadau wote kuongeza juhudi katika kuleta usawa wa kijinsia ili kumwondolea mwanamke vikwazo vinavyomrudisha nyuma kimaendeleo, anaandika Happyness Lidwino.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Grace Kisetu, Kaimu Mkurugenzi TGNP wakati wa maadhimisho siku ya wanawake duniani ambayo kilele chake ni tarehe 8 Machi mwaka huu.

TGNP kwa kishirikiana na wadau wengine wa kutetea haki za wananwake jinsia na watoto wameeleza kuwa, kuna changamoto katika kufikia usawa wa kijinsia.

Na kwamba inapaswa kutazama ukatili wa kijinsia na jinsi unavyowaathiri wanawake na watoto katika kufikia ndoto zao.

Amesema, kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni ‘50 kwa 50 kufikia 2030 Inawezekana, Tuongeze Juhudi.”

Licha ya kuwapo kwa kauli hiyo, TGNP bado wanalia na unyanyasaji wa kijinsia hususani suala la ukeketaji unaoendelea nchini.

Grace amesema, vikwazo vilivyopo ni pamoja na ukatili wa kijinsia ikiwemo ukeketaji, mimba na ndoa za utotoni ambazo humkwamisha  mtoto wa kike kufikia ndoto zake za elimu na uongozi.

“Tunaamini kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya ukatili wa kijinsia na uongozi kwa wanawake na watoto wa kike. Mfano; katika Baraza la Mawaziri 16 wanne pekee ndio wanawake.

“Kati ya madiwani 3957 wanawake ni 198 tu ukija katika bunge wanawake ni asilimia 36.9 pekee. Katika masuala ya uongozi wanawake wapo nyuma bado,” amesema Kisetu.

Kisetu amesema wakati siku ya wanawake duniani ikisherehekewa, serikali inatakiwa itafakari vikwanzo vya mwanamke ikiwemo ya umiliki wa ardhi na kwamba licha ya kuwepo kwa sheria zinazomlinda mwanamke kujipatia na kumiliki ardhi lakini bado wanabaguliwa na kunyimwa haki zao.

“Vile vile bado kuna mifumo kandamizi inayomweka mwanamke pembezoni katika masuala ya elimu ngazi zote. Hata ufaulu kati ya mwanamke na mwanaume  wanawake wapo nyuma kutokana na vikwazo mbalimbali kama vyoo, maji, mabweni, ukosefu wa vifaa vya kumsaidia mwanamke wakati wa hedhi,”

error: Content is protected !!