July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TGNP: Tunataka nafasi moja muhimu

Makamu wa Rais, Gharib Bilali akichukua fomu ya uwania Urais

Spread the love

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) umesema kuwa, hautakuwa tayari kuunga mkono watangaza nia au chama chochote cha siasa ambacho katika sera zake hakitaonesha mrengo wa kijinsia katika kutetea haki za wanawake, watoto, walemavu na vijana. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji TGNP, Lilian Liundi wakati wa warsha ya siku mbili ya waandishi wa habari iliyolenga kujenga uelewa wa pamoja kuhusu dhana ya kijinsia.

Amesema kuwa, ni vema vyama vya siasa vikaweka uwiano sawa katika rasilimali zinazotumika kutangaza nia ili kuwapa fursa wanawake walio na uwezo wa kuongoza na hawana rasilimali za kutosha kutangaza nia.

Ameongeza kuwa, TGNP haitakuwa tayari kuwaunga mkono wanasiasa ambao hawataonesha nia ya kutatua matatizo ya kijinsia.

“Tunataka watamke rasmi kwamba, nafasi moja wapo kati ya tatu za juu kwa watakaoshika madaraka zichukuliwe na wanawake…. namaanisha Waziri Mkuu, Makamu wa Rais au Rais awe mwanamke,” amesema Liundi.

Katika masuala ya bajeti amesema, kila wizara husika zitamke wazi uwiano wa kijinsia katika makundi husika pamoja na kutaja fungu lilotengwa kwa kila kundi.

Mkurugenzi wa Bodi ya TGNP, Vicencia Shule amesema kuwa, wanachi wanatakiwa kuwa makini kwani viongozi wengi wamekuwa wakitumia rasilimali kubwa katika mambo yao ya kisiasa kuliko kusaidia huduma za kijamii.

Hata hivyo, ametoa rai kwa wanawake waliopata nyadhafa za juu na kupata bahati ya kuingia katika mabaraza ya bajeti, kuyapa kipaumbele makundi maalum ili kuwakomboa wanawake walio nyuma yao. 

error: Content is protected !!