Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko TFS yaweka mpaka Msitu wa Kuni Morogoro
Habari Mchanganyiko

TFS yaweka mpaka Msitu wa Kuni Morogoro

Spread the love

 

WAKALA wa Hifadhi ya Misitu Tanzania (TFS) imeanza zoezi la kuweka mpaka katika Msitu wa Morogoro maarufu Msitu wa Kuni uliopo Wilayani Mvomero kwa lengo la kuulinda dhidi ya wavamizi. Anaripoti Jonas Mushi, Morogoro … (endelea).

Zoezi hilo ni utekelezaji wa maagizo ya kamati ya Mawaziri nane iliyofika katika eneo hilo tarehe 26, Mei mwaka huu na kufanya tathimini ya uharibifu wa eneo hilo linalotegemewa kwa uhifadhi wa mazingira na miti.

Akizungumza jana wakati wa zoezi la kuchonga barabara ambayo ndiyo itateganisha eneo la makazi na msitu huo, Afisa Misitu Mwandamizi wa Msitu wa Morogoro, Kelesi Mwaijele, amesema wanaendelea na zoezi la uwekaji mpaka wa hifadhi ili kutenga eneo lililomegwa na kuachwa kwa wananchi waliokuwa wamelivamia.

“Zoezi hili ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali kutenganisha maeneo ya misitu na lile ambalo litachukuliwa na Serikali kwa matumizi mengine,” alisema Mwaijele ambaye alikuwa nasimamia uwekaji mpaka huo.

Amesema sababu hasa za kuamua kuweka mpaka ni kutokana na eneo la msitu kuendelea kuvamiwa na wananchi kinyume cha sheria na kusababisha athari kubwa “kuna maeneo yamevamiwa wamekata miti, wameingiza mifugo, kuchoma mkaa, ujenzi wa makazi holela yasiyo na mipango wala kibali.”

Amesema licha juhudi za mara kwa mara za kuwaondoa wavamizi katika eneo hilo lakini wamekuwa wakijirudia na kuvamia tena.

Amesema hivi sasa wamejipanga kwa kuanza kuweka kwanza mipaka kwa kuchinga barabara na baadae wataweka mabango na kuanza kupanda miti kwenye eneo hilo.

Amesema kutokana na wananchi kuvamia msitu huo kumesababisha athari za kimazingira ikiwemo kutoweka kwa miti ya asili ikiwemo mninga, mpingo na acacia.

Akizungumza hivi karibuni na wananchi wa mtaa wa CCT ambao awali lilikuwa ni hifadhi ya Msitu wa Morogoro, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatma Mwassa alisema wananchi wote ambao watakuwa ndani ya mpaka wataondolewa.

“Tunakwenda kuwaonesha mpaka mpya ikiwa umeangukia upande ambao ndiyo tumeruhusiwa kuutumia, jua tutakupimia, tutakumilikisha lakini kwa kulipia. Ukiwa umeangukia kwenye hifadhi anza kuvunja mwenyewe chukua tofali lako moja moja tutii sheria bila shuruti,” alisema Mwassa.

Mkuu huyo wa mkoa alikemea vitendo vya kuvamia maeneo na kujenga bila kufuata sheria na utaratibu na kubainisha kuwa wengine wanaofanya hivyo ni maofisa wa Serikali amabao wana uelewa.

“Morogoro tuache mambo tunayofanya yanatia aibu, msifanye mambo ya hovyo halafu mkasingizia watu ubaya. Na kwenye ule msitu wengine ni maafisa wakubwa wa Serikali na wanajenga usiku sasa hao hawajui wanachofanya,” alisema.

Alibainisha kuwa ili kujenga nyumba ni lazima mwananchi awe na hati miliki ya Ardhi na pili kuwa kupata kibali cha ujenzi wa nyumba anayotaka kujenga na vyote hivyo vinapatikana Ofisi za Ardhi za Halmashauri husika na sio kwa Mtendaji wa Kijiji wala Mtaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!