July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TFS watimua wafugaji ndani ya hifadhi Ikowa

Moja ya misitu iliyopo nchini Tanzania

Spread the love

MENEJA wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Kanda ya Kati, Mathew Kiondo ametoa siku mbili kwa wafugaji wanaolisha mifugo yao katika Msitu wa Ikowa wilayani Chaminwo jijini Dodoma kuondoka haraka. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Sambamba na hilo, pia amewataka watu waliojenga nyumba na kuishi katika msitu huo nao kuondoka mara moja ili kuhimarisha utunzaji wa msitu huo.

Meneja huyo ametoa kauli hiyo leo tarehe 1 Aprili 2019 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Upandaji Miti duniani ambapo TFS, Kanda ya Kati imeweza kupanda miti 1200 katika Msitu wa Ikowa kwa lengo la kufanya Dodoma kuwa ya kijani.

Kiondo kwa kushirikiana na watumishi wa TFS na wananchi katika kupanda miti amesema, haiwezekani serikali ikawachekea watu ambao wanahusika katika kuharibu mazingira.

“Sasa viongozi wa Kata ya Manchali na vijijini jirani nawaagiza, hakikisha mnawaondoa wafugaji ambao wanalisha mifugo yao katika msitu huu.

“Pia kuna watu ambao wamefyeka msitu na kulima mahindi na mazao mengine, sasa natoa agizo kuwa watu hao waliolima mazao hayo wapewe miti wapande katika maeneo hayo, “amesema Kiondo.

Mary Mazengo, Diwani wa Kata ya Manchali (CCM) amesema kuwa, hatafumbia macho maagizo ya Meneja wa TFS wa Kanda ya Kati.

Amesema, licha ya kuwa ni mwanasiasa lakini utunzaji wa mazingira hautaji siasa, hivyo kila ambaye anajitambua kuwa anafanya shughuli za kibinadamu katika msitu huo, aondoke.

error: Content is protected !!