SHIRIKISHO la Mpira wa Miguuu Tanzania (TFF), limewataka wadau mbalimbali wa mchezo huo pamoja na wagombea waliojitokeza kwenye zoezi la uchukuaji fomu kwa ajili ya uchaguzi Mkuu kufuata taratibu na kanuni za uchaguzi ili kuondoa migogoro. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Rai hiyo imetolewa na katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Kidao Wilfred, kwenye makao makuu ya TFF, Karume Ilala Jijini Dar es Salaam.
Katibu huyo alitoa tahadhari kwa wadau wa mpira wa miguu kwa kuwataka, waiachie Kamati ya Uchaguzi ya TFF ifanye kazi yake mpaka zoezi hilo litakapoisha, bila kuwaingilia.
Aidha Kidao aliendelea kufunguka kuwa kama mchakato huo utaingiliwa basi kuna athari kubwa kama nchi, kupoteza vitu vingi kutoka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), na Shirikisho la Mpira Duniani (FIFA), na kusisitiza kuwa kamati hiyo haitakiwi kuingiliwa na mtu yoyote kwa mujibu wa katiba ya TFF.
“Mchakato unaendeshwa kwa mujibu wa katiba ya TFF, sio Kidao wala Rais wa TFF anayepaswa kuingilia.
“Mchakato ukiingiliwa athari ya kwanza ni TFF kusimamishwa kwa uwanachama na Fifa, na timu za Taifa hazitaweza kushiriki mashindano ambayo yanaandaliwa na Caf pamoja na Fifa,” alisema Kidao
Leave a comment