Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari TFF yawalima faini Manara, Bumbuli
HabariMichezo

TFF yawalima faini Manara, Bumbuli

Spread the love

MAAFISA kutoka Idara ya Habari na mawasilinao ya klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli na Haji Manara wametozwa faini ya shilingi 500,000 na kamati ya usimamizi na uwendeshaji wa Ligi (Kamati ya Saa 72) kufuatia kuwashtumu waamuzi kwenye vyombo vya habari. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Wawili hao waliitisha mkutano na waandishi wa habari tarehe 8 Februari 2022 kwenye makao makuu ya klabu hiyo, huku wakionesha masikitiko yao ya kutokubaliana na mwenendo wa waamuzi kwa baadhi ya michezo ya LigiKuu Tanzania Bara.

Katika mkutano huo Afisa Habari wa klabu hiyo Hassan Bumbuli amesema kuwa, kuna baadhi ya maamuzi ambayo yanaonekana kunufaisha baadhi ya timu na kuumiza timu nyingine.

“Kumekuwa na mlolongo wa matukio ya maamuzi yenye utata ambayo kwa namna moja au nyingine yananyima haki ya timu zingine na yanatoa manufaa kwa timu zingine,”Alisema Bumbuli.

Kwa upande wa msemaji wa klabu hiyo ambaop ni vinara wa Ligi Kuu mpaka sasa, Haji Manara kwa upande wake alitaka haki itendeke kwa kila upande, licha ya kuona kwa upande wao wanaadhibiwa kila wakifanya makosa lakini ni tofauti inavyokuwa kwa upande wa Simba.

“Tunataka kuwa waamuzi kuwa na haki kwanini Yanga ikifanya makosa iadhibiwe lakini wenzetu pia Simba wakifanya makosa basi haki itendeke kwanini wao wakifanya makosa haki haitendeki.” Alisema msemaji huyo

Licha ya kupigwa faini kwa kutakiwa kulipa kiasi hiko cha fedha, wawili hao wamepewa onyo kali na kamati hiyo katika kosa hilo walilotenda.

Katika hatua nyingine kamati hiyo ilimuondoa katika orodha ya waamuzi kwa mizunguko mitatu, aliyekuwa mwamuzi wa kati wa mchezo kati ya Simba dhidi ya Tanzania Prison Ahmada Simba kwa kushindwa kutafsiri sharia za mchezo wa soka.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

error: Content is protected !!