April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TFF yatoa kauli uchaguzi mkuu Yanga

Makao Makuu ya Klabu ya Yanga

Spread the love

KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), chini ya Mwenyekiti wake Wakili Ali Mchungahela imetangaza tarehe 5, Mei 2019 ndiyo siku utakaofanyika uchaguzi mkuu wa klabu ya Yanga badala ya 28 April mwaka huu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea)

Wakili huyo amesema kuwa uchaguzi wa klabu hiyo kwa sasa utasimamiwa na pande zote mbili yaani Yanga ambao ni wahusika na TFF ambao ni wasimamizi na fomu kwa wagombea zitaanza kutolewa April 2, mwaka huu.

“Tarehe ya uchaguzi mwenye mamlaka ya kuitangaza ni kamati ya uchaguzi ya TFF ambaye mwenyekiti wake ni mimi, mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ndani ya Yanga yeye aliongea mapendekezo yake na ukizingatia hiyo tarehe 28 April itakuwa fainali ya AFCON kwa vijana,” alisema Wakili Mchungahela.

Aidha wakili huyo aliongezea kuwa wale wagombea waliochukua fomu hapo awali kabla ya uchaguzi kusimamishwa wataendelea na mchakato na wagombea wapya watakaojitokeza kwa kuwa walisha kizi vigezo hapo awali.

Klabu hiyo inakwenda kufanya uchaguzi huo ambao utampata Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti pamoja na wajumbe wa kamati ya utendaji, baada ya waliotangulia kujiuzuru.

Tazama video kamili hapo chini

error: Content is protected !!