May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TFF yashusha Nyundo kwa viongozi wa soka

Ofisi za TFF

Spread the love

 

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewafungia Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Shinyanga (SHIREFA), Bannister Misango kutojihusisha na soka kwa miaka miwili mara baada ya kufanya kosa la kimaadili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kiongozi huyo ambaye amefungiwa kupitia Kamati ya Maadili ya TFF mara baada ya kutofanya kazi yake kwa uweledi kwa kukiuka katiba ya SHIREFA ibara 41(10).

Mwaka 2009 Misango alifanya kosa kwa kumteua mwakilishi wa klabu, Michael Kaijage kuwa kaimu katibu mkuu badala ya katibu msaidizi wa chama hicho, Stephen Mihambo na kukili kosa hilo mbele ya kamati ya maadili.

Taarifa kutoka TFF imeleza kuwa, mwenyekiti huyo amepewa adhabu hiyo kwa kuzingatia ibara ya 2(6)(1) na ibara ya 3(9)(1) za mwongozo wa maadili ya TFF toleo la 2013.

Aidha kamati hiyo pia imewafungia Dikson Mulimuka, mgombea wa nafasi ya mwenyekiti chama cha soka mkoa wa Tabora (TAREFA) pamoja na kiongozi wa chama hicho, Stella Maganga kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa miaka 10.

Dikson Mulimuka ambaye alikuwa mgombea kwenye uchaguzi wa Tarefa, alifanya kosa kwa kusimamia uchaguzi wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Urambo, jambo ambalo ni kinyume na ibara ya 19(2) ya mwongozo wa maadili ya TFF toleo la 2013.

Kwa upande wa Stella Maganga ambaye ni kiongozi wa Tarefa, alifungiwa na kamati hiyo ya maadili baada kwa kuwa mgombea, msimamizi na mpiga kura kwenye uchaguzi wa chama cha mpira wa miguu Wilaya ya Sikonge kinyume na ibara ya 3(3.1) ya mwongozo qa maadili ya TFF, toleo la 2013.

error: Content is protected !!