December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TFF yaruhusu mechi za kirafiki

Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imeruhusu kuendelea kwa michezo ya kirafiki kwa klabu kwenye ngazi husika kwa kibali maalumu, ili kuhakikisha wanafuata muongozo wa kujikinga na ugonjwa wa Covid 19 katika michezo hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Tarehe 8 Juni, 2020, TFF iliwaita viongozi wa klabu za Simba, Yanga, Azam, KMC pamoja na Transit Camp ambao walicheza michezo ya kirafiki hivi karibuni katika maandalizi kuelekea michezo ya Ligi Kuu inayotarajia kuanza Juni 13 mwaka huu.

Katika michezo hiyo, ilionekana dosari kubwa katika upande wa mashabiki kwa kushindwa kufuata muongozo wa serikali kupitia Wizara ya Afya sambamba na Wizara ya michezo juu ya taratibu za kufuata kwenye michezo hiyo.

Muongozo huo umeeleza kuwa mashabiki wanapaswa kunawa mikono kabla ya kuingia uwanjani sanjari na kuvaa barakoa pamoja na kukaa umbali wa mita moja (social distance) wakati wa mchezo.

 

Katika kikao hicho klabu zilikubaliana na TFF kufuata muongozo wa Serikali katika hatua ya kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19, kwa kuweka watu maalumu majukwaani ambao watakuwa wakisimamia na kuwapanga mashabiki namna ya kukaa.

Baada ya mashauliano hayo TFF imeruhusu kuchezwa kwa mchezo kati ya Azam dhidi ya KMC utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Chamazi, na kutumika kama mfano.

Aidha shirikisho hilo limesema kuwa Uwanja wa MO Simba Arena hautatumika kwa michezo ya kirafiki kwa vile uwanja huo ni maalumu kwa ajili ya mazoezi.

error: Content is protected !!