February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TFF yapangua tena ratiba ya Ligi Kuu Bara

Spread the love

MICHEZO namba 14 na 19 ya Ligi Kuu Bara kati ya mabingwa watetezi Simba na Mbeya City na ule wa Azam FC dhidi ya Ndanda itachezwa siku ya Jumatatu 27 Agosti, 2018 badala ya 25 Agosti, 2018 kama ilivyopangwa hapo awali kutokana na mabadiliko yaliyofanywa na bodi ya ligi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Katika sehemu ya barua iliyotoka bodi ya ligi iliyosainiwa na Mwenyekiti wake Boniface Wambura imeonesha sababu za kusogeza michezo hiyo mbele ni kupisha maandalizi ya mchezo wa fainali wa kombe la CECAFA U-17.

“Mabadiliko haya yametokana na Uwanja wa Taifa kufanyika maandalizi kwa mchezo wa fainali za CECAFA U-17 ambao utachezwa tarehe 26.08.2018 (Jumapili)”

Hii ni mara ya pili kwa bodi ya ligi kupangua michezo ya Ligi Kuu kwa msimu huu wa 2018/19 kutokana na sababu za kuingiliana kwa shughuli za matumizi ya viwanja na hali hiyo inatokea kutokana na 90% ya klabu zinazoshiliki ligi hiyo havina viwanja vyao binafsi.

error: Content is protected !!