April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TFF yamtimua Amunike, kutangaza mrithi wake

Emmanuel Amunike, aliyekuwa Kocha wa Taifa Stars

Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imesitisha mkataba wa Kocha wa Timu ya Taifa “Taifa Stars” Emmanuel Amunike baada ya timu hiyo kuondoshwa katika hatua ya makundi ya Fainali za Mataifa Afrika (AFCON 2o19). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa iliyotolewa na TFF imesema kuwa shirikisho hilo limefikia makubaliano ya pamoja kusitisha mkataba kati yao na Amunike.

TFF itatangaza Kocha wa muda atakayekiongoza Kikosi cha Timu ya Taifa kwa mechi za CHAN.

Makocha wa muda watatangazwa baada ya Kamati ya Dharura ya Kamati ya Utendaji (Emergency Committee) itakapokutana Julai 11,2019.

Mchakato wa kutafuta Kocha mpya umeanza mara moja.

error: Content is protected !!