May 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TFF yampiga nyundo aliyekuwa kocha Yanga

Lucy Eymael

Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemfungia kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya Sh. 8 milioni, aliyekuwa kocha wa Yanga, Luc Eymael kwa kutoa maneno ya uchochezi na ubaguzi kwa wadau na mshabiki wa soka nchini. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kocha huyo ambaye ni raia wa Ubelgiji, amepewa adhabu hiyo kufuatia kutamka maneno yenye viashilia vya ubaguzi kwa mashabiki wa klabu hiyo kupitia kipande cha sauti yake (audio clip) iliyokuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii mara baada ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara kumalizika kati ya Lipuli dhidi ya Yanga.

Kamati hiyo imechukua hatua hiyo huku Luc Eymael akiwa hayuko nchini mara baada ya waajili wake klabu ya Yanga kumtimua kazi na kumtaka kuondoka nchini ndani ya siku mbili toka alipofanya kosa hilo.

Moja ya kauli iliyosikika na kuibua hisia za wengi kwenye kipande hiko cha sauti ni kuwafananisha kelele za mashabiki wa klabu hiyo kama sauti za manyani.

Kocha huyo alijiunga na Yanga januari mwaka huu na kuingoza timu hiyo kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kuifikisha hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho (FA)

error: Content is protected !!