Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo TFF yaianika Lipuli, inadai milioni moja tu
Michezo

TFF yaianika Lipuli, inadai milioni moja tu

Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa ufanunuzi juu ya sakata la kudaiwa na klabu ya Lipuli FC kiasi cha Sh. 10,000,000 (milioni kumi) mara baada ya kushika nafasi ya pili kwenye Kombe la Shirikisho (FA) na kueleza kuwa klabu hiyo inaidai Sh. 1,000,000 (milioni moja tu) huku fedha nyingine walikatwa baada kuwa na madeni. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Klabu hiyo ilishika nafasi hiyo ya pili mara baada ya kupoteza kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Azam FC kwa bao 1-0, katika mchezo uliofanyika tarehe 1 juni, 2019 Kwenye Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi kwenye msimu wa 2018/19.

Hivi karibuni klabu hiyo ilitoa malalamiko kuhusu kutopokea kiasi hicho cha fedha ambacho kinatolewa na mdhamini wa michuano hiyo kampuni ya Azam Media na kuiandikia barua TFF kukumbushia jambo hilo na shirikisho hilo iliwajibu kukili kupokea barua yao kupitia barua yenye kumbukumbu namba TFF/ADM/GS.DEPT.20/224 ya tarehe 14 Juni, 2020 na kuelezwa kuwa watalipwa hivi karibuni.

Walace Karia, Rais wa TFF

Baada ya kuendelea kwa sintofahamu kuhusu malipo ya fedha hizo kutoka kwa viongozi wa Lipuli, leo tarehe 28 Desemba, 2020 TFF kupitia taarifa waliyoitoa ilieleza kuwa klabu hiyo imeshalipwa kiasi cha Sh. 5 milioni katika kiasi cha Sh. 10 milioni wanazodai kama zawadi baada ya kushika nafasi ya pili.

Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa shirikisho hilo liliwakata Lipuli Sh. 4 milioni kama deni mara baada ya kubainika kutowalipia ada wachezaji wao wawili wa kigeni waliowasajili kwenye msimu wa 2018/19.

TFF imeleza kuwa mpaka sasa wanadaiwa na klabu hiyo kiasi cha Sh. 1,000,000 itakayolipwa hivi karibuni.

Klabu hiyo ambayo maskani yake mkoani Iringa kwa sasa inashiriki ligi daraja la kwanza mara baada ya kuporomoka kutoka Ligi Kuu kwenye msimu uliopita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Michezo

TFF, Amrouche ngoma nzito

Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...

error: Content is protected !!