
Ramadhan Singano 'Messi' akiitumikia klabu yake ya Simba
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefuta mikataba yote miwili yenye utata, kati ya ule wa Ramadhani Singano ‘Messi’ na mkataba waliokuwa nao klabu ya Simba.
Klabu ya Simba iliingia kwenye mgogoro na mchezaji wake Messi kuhusu mwisho wa mkataba wa nyota huyo kuitumikia timu hiyo, ambapo mchezaji alikuwa ana mkataba unamalizika mwisho mwa msimu huu, huku klabu ikiwa na mkataba wa msimu mmoja zaidi.
Pande zote mbili leo zilikutana TFF ambapo baada ya kuzisikiliza pande zote mbili, maamuzi yaliyoamuliwa ni kufuta mikataba yote miwili kati ya Messi na Simba.
Baada ya kikao kirefu muafaka uliofikiwa chini ya TFF ni kwamba mkataba wa alionao Messi uvunjwe na mkataba walionao Simba uvunjwe waingie makubaliano mapya.
Upande wake, Singano hajakubaliana na maamuzi hayo kwa sababu unamtaka yeye akubaliane na Simba tena. Lakini kwa mujibu wake ni kwamba anatakiwa kuwa huru kama mkataba umevunjwa na sio kukubaliana upya na Simba.
More Stories
Injinia Hersi kuanza na uwanja Yanga
Sopu aibuka kinara wa mabao ASFC
Mgunda atoa tahadhari kwa Mayele kesho