SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefungua rasmi dirisha kubwa la usajili litakalodumu kwa siku 42, baada ya kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2020/21. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Dirisha hilo la usajili litahusu timu ziunazoshiriki Ligi Kuu. Ligi daraja la kwanza na la pili pamoja na Ligi Kuu ya wanawake.
Katika taarifa iliyotolewa na TFF, imeeleza kuwa dirisha hilo, limefunguliwa kuanzia leo tarehe 19 Julai, 2021 na litafungwa tarehe 31 Agosti, 2021.
Wakati taarifa hiyo ikitoka tayari klabu mbalimbali za Ligi tayari zilishaanza usajili wakati msimu ukielekea mwishoni.
Klabu za Simba, Yanga na Azam FC tayari walishaanza kufanya hivyo kwa kuwasainisha baadhi ya wachezaji kwa mikataba ya awali.
Mpaka sasa klabu ya Yanga imeshakamlisha usajili wa beki wa kulia kutoka Jamhuri ya Congo, Djuma Shaban ambaye alikuwa anakipiga kwenye klabu ya AS Vita.
Kwa upande wa Azam FC wao mpaka sasa wamekamilisha usajili wa wachezaji wawili kutoka Zambia, ambao ni Charles Zulu, aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Cape Town City inayoshiriki Ligi Kuu nchini Afrika Kusini na mwengine ni Paul Katema kutoka kwenye klabu ya Red Arrows.
Leave a comment