May 16, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TFF yafungua dirisha la usajili

Alfred Lucas, msemaji wa TFF

Spread the love

SHIRIKISHO la soka nchini Tanzania (TFF), limetangaza kufungua rasmi dirisha la usajili wa wachezaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara, 2017/2018 kuanzia leo 15 Juni mpaka tarehe 6 Agosti, 2017, anaandika Shafiyu Kyagulani.

Alfred Lucas, msemaji wa TFF amewambia wanahabari kuwa kufunguliwa kwa dirisha la usajili kutatoa fursa kwa klabu za ligi kuu kufanya usajili ingawa tayari baadhi ya klabu zilishaanza kusajili kabla ya ufunguzi wa dirisha hilo.

Tayari klabu ya Yanga imeripotiwa kumnasa Abdallah Ally Shaib (Ninja) kutoka Jang’ombe FC ya Zanzibar huku Kagera Sugar ikimsajili beki wa kati Juma Nyoso na Simba SC wakiripotiwa kuwanasa John Bocco, Shomari Kapombe na mlinda mlango Aishi Manula – wote kutoka Azam FC.

error: Content is protected !!