July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TFF yafikishwa Mahakamani

Walace Karia, Rais wa TFF

Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imepokea kesi ya kupinga uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), iliyofunguliwa na Ally Saleh ‘Alberto’ ambaye alikuwa moja ya wagombea kwenye uchaguzi huo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika tarehe 8 Agosti, 2021, jijini Tanga, ambapo mpaka sasa kamati ya uchaguzi imempitisha Wallace Karia kuwa mgombea pekee kwenye nafasi ya Urais.

Ally Saleh ‘Alberto’

Kesi hiyo ya madai namba 98 ya mwaka 2021, iliyofunguliwa na Ally Salehe, raia wa Tanzania anayeishi Zanzibar ambayo itakuwa chini ya Jaji Kakolaki ambapo wadai ni TFF, Bodi ya wadhamini na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Wakili Kiomoni Kibamba.

Mahakama hiyo pia imewataka wadaiwa hao wote watatu kufika kesho mahakamani hapo, kujibu hoja ya kwanini uchaguzi huo usisimamishwe.

error: Content is protected !!