Monday , 27 May 2024
Home Kitengo Michezo TFF wazikumbusha klabu zisizokamilisha usajili wa kieletroniki
Michezo

TFF wazikumbusha klabu zisizokamilisha usajili wa kieletroniki

Cliford Ndimbo, Msemaji wa TFF
Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linavikumbusha klabu za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili ambavyo havijafanya usajili kupitia mfumo wa usajili wa TFF FIFA Connect kufanya usajili wao. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Klabu ambazo bado hazijafanya usajili wawasiliane na TFF kama kuna msaada wowote wanahitaji ili kukamilisha usajili wao.

Dirisha la Usajili litafungwa Alhamisi Julai 26, 2018 na TFF inasisitiza hakutakuwa na muda wa ziada katika usajili.Timu ambayo itashindwa kukamilisha usajili haitaruhusiwa kushiriki Ligi ya msimu ujao wa 2018/2019.

Klabu za Ligi Kuu ambazo hazikamilisha usajili bado ni Ruvu Shooting, Mbeya City, Tanzania Prisons, Mtibwa Sugar, Mwadui, Kagera Sugar, Alliance, Lipuli, African Lyon, KMC na Azam FC.

Kwa upande wa ligi daraja la kwanza klabu ambazo hazijakamilisha usajili ni Ashanti United, Boma FC, Friends Rangers, Green Warriors, Kiluvya United, Majimaji FC, Mashujaa FC, Mawenzi Market, Mbeya Kwanza, Mgambo Shooting, Njombe Mji, Pamba FC, Dar City na Polisi Tanzania.

Klabu za daraja la pili ambazo hazijakamilisha ni Area C United, Changanyikeni, Cosmopolitan FC, Kumuyange FC, Gipco FC, Mirambo FC, Madini FC, Mkamba Rangers, Mvuvumwa, Polisi Dar, The Mighty Elephant, Toto African, Villa Squad, Majimaji Rangers, Mtwivila City, Kasulu Red Star na Sahare All Stars.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa  Ligi Kuu ya NBC, yaahidi maboresha zaidi

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League),...

Michezo

Unamalizaje Jumapili hujabeti na Meridianbet?

Spread the love JUMAPILI ya leo tutashuhudia mitanange kibao ambayo itamalizika kuanzia...

Michezo

Jipigie pesa na Meridianbet leo hii

Spread the love KAMPUNI kubwa ya ubashiri Tanzania inakwambia hivi huu ndio...

Michezo

Endelea kubashiri na Meridianbet, Ligi bado zipo

Spread the love BAADA ya ligi mbalimbali kutamatika, bado kuna ligi mbalimbali...

error: Content is protected !!