August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TFF waishangaa BMT kuzuia uchaguzi

Celestine Mwesigwa, Katibu Mkuu wa TFF

Spread the love

WAKATI serikali ikikataza uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuwa halikushirikishwa kwa kuwa wao ndio wasimamizi wakuu, Celestine Mwesigwa, Katibu Mkuu wa shirikisho hilo amesema Katiba yao haiingiliani na serikali, anaandika Shafiyu Kyagulani.

Baraza la michezo nchini (BMT), lilitoa liliandika barua kwa TFF jana kuzuia uchaguzi huo uliotarajiwa kufantika Agosti 12, mwaka huu kwani wao ndio wasimamizi wa michezo yote nchini.

“Katiba ya TFF wala hailiingiliani na Baraza la Michezo nchini.” Kauli hiyo inaashiria kuwa TFF imeshangazwa na barua hiyo.

BMT imeomba kukutana na TFF ili wajadili mambo kadhaa ifikapo Julai 1, 2017. Baraza hilo limesema kuwa, klabu, vyama na mashirikisho ya michezo yameundwa chini ya sheria ya baraza la michezo la Taifa Na 12 ya 1967 na Marekebisho Na 6 ya 1971 pamoja na kanuni za usajili Na.442 za mwaka 1999, na kuwataka TFF wafuate utaratibu wa uchaguzi wa viongozi uliofafanuliwa kwenye sera ya maendeleo ya michezo Ibara 5;2;2.

Wakati sakata hilo likitokea Emmanuel Kuuli, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, alishatangaza wanaotaka kugombea nafasi hizo wakae tayari.

error: Content is protected !!