July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TFF, Simba, Yanga watakiwa kulipa kodi TRA

Spread the love

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuzisimamia klabu zake kushiriki kulipa kodi ili kuongeza mapato ya taifa. Anaandika Hamisi Mguta …(endelea).

Rai hiyo imetolewa na TRA katika semina ya ulipaji wa kodi ya mapato iliyoendeshwa na shirika hilo sambamba na TFF juu ya sheria mpya ya ulipaji kodi ya mwaka 2014 na iliyoanza kutumika rasmi Julai mosi mwaka huu.

Semina hiyo imehudhuliwa na viongozi wa TFF, viongozi wa baadhi ya klabu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara na wadau wa soka, iliyohusisha sheria ya ulipaji kodi.

Afisa Kodi Mwandamizi wa TRA, Donasian Assey amesema sehemu kubwa ya ongezeko la pato la taifa linatokana na ulipaji wa kodi ya mapato, hivyo klabu zinapaswa kujisajili katika mfumo wa ulipaji wa kodi.

Assey amesema klabu nyingi zinapata mapato kwa kuvaa jezi zenye matangazo ya makampuni ambazo zinawalipa timu, hivyo klabu zinatakiwa kulipa kodi kutokana na kipato wanachopata kutoka kwa makampuni wanayowadhamini.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Martin Chacha amesema semina hiyo imekuwa na msaada mkubwa kwa TFF na klabu, kwani wamepata uelewa juu ya ulipaji wa kodi na kufahamu sheria mpya ya ulipaji wa kodi.

error: Content is protected !!