January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TFDA yatekeza pombe ‘fake’ za Sh. 83 mil

Spread the love

MAMLAKA ya Chakula na Dawa Kanda ya Ziwa (TFDA) imetekeza pombe `fake` aina ya Empire, Singnature Vodka na bidhaa nyingine zenye thamani ya zaidi ya Sh. 83 milioni zilikokuwa zinatengenezwa na kiwanda cha Simba gin cha jijini hapa. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Mkuu wa Ukaguzi wa TFDA Mkoa wa Mwanza, Julius Timothy, amesema pombe hizo zilizotekezwa zilikuwa ni tani 15.18 ambazo zilikuwa zimefichwa katika kiwanda hicho na baada ya wasamalia wema kutoa taarifa walifakiwa kuzikamata.

Timothy amesema wamiliki wa kiwanda hicho pia waliamua kutumia nembo ya nchini Uganda ili kuwaaminisha wananchi kwamba bidhaa hizo ni halali kwa matumizi ndivyo sivyo ambako ni kinyume na sheria.

“Baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi, tulifika katika kiwanda hicho ambako tulikuta bidhaa mbalimbali ikiwamo pombe aina ya Empire na Signature Vodka, tulifanikiwa kuzikamata na kibaya zaidi wanatumia nembo ya Uganda,” amesema Timothy.

Hata hivyo Timothy amesema kutokana na kiwanda hicho kuendesha shughuli zao kinyume na utaratibu. Wamekifungia kiwanda hicho kwa muda wa miezi miwili mpaka pale taratibu za kisheria zitakapokamilika.

Kaimu Afisa Afya kutoka Jiji la Mwanza, Sophia Kiluvia, amesema TFDA imefanya kazi kubwa kuokoa uhai wa binadamu kutokana na bidhaa hizo kuwa hazijapimwa, kuendelea na uchunguzi huo utaweza kupunguza bidhaa ambazo ni `fake`.

Amesema katika kipindi hiki kumeongezeka kwa viwanda bubu vingi vinavyoweza kuhatarisha maisha ya binadamu, hivyo kama serikali wanaowajibu wa kushirikiana na wananchi kuhakikisha wanatokomeza tatizo hilo.

error: Content is protected !!