January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TFDA yakamata vipodozi haramu vya Sh. mil. 135

Spread the love

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na Shirikisho la Polisi wa Kimataifa (Interpol) imesema, vipodozi haramu ilivyovikamata kwenye opereshemi yake ya siku tatu vilikuwa na thamani ya Shilingi  Milion 135. Operesheni hiyo ilifanyika kuanzia Agosti 19 na kukamilika Agosti 21. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Oparesheni hiyo pia ilifanyika katika nchi nane zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo ni  Afrika kusuni, Zimbabwe, Malawi, Msumbiji, Swaziland, Zambia na Angola ikiwemo Tanzania.

Kwa upande wa Tanzania oparesheni hiyo ilifanyika katika Mikoa minane ambayo ilionekana kukithiri kwa biashara hiyo haramu. Mikoa hiyo ni Mbeya, Mtwara, Mwanza, Mara, Arusha, Kilimanjaro, Dodoma na Dar es Salaam.

Katika mkutano wake leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa  TFDA Hiiti Sillo amesema, maeneo yaliyokaguliwa na kupatikana kwa dawa na vipodozi hivyo ni kwenye Maduka ya Madawa, maduka ya jumla na rejareja ya vipodozi, Hospitalini, vituo vya afya, maduka ya serikali na waingizaji wa vipodozi na dawa.

Sillo amesema jumla ya maeneo 243 yalikaguliwa katika oparesheni hiyo ambapo kwa upande wa Dar es Salaam walikagua maeneo 115, Mtwara 17, Kilimanjaro 13, Arusha 12, Mara 18, Mwanza 27 Mbeya 16 na Dodoma 16.

Amesema miongoni mwa dawa zilizokamatwa ni pamoja na zile zilizoisha muda wa matumizi aina 35 zenye thamani Sh.1,517,500, Dawa za Serikali katika maduka ya watu aina tatu zenye thamani ya Sh.98,250, Dawa za Serikali ya Kenya aina nne zenye thamani ya Sh.170,000, Dawa ambazo hazijasajiliwa aina 97 zenye thamani ya Sh.21,526, 400, Dawa zilizo kutwa kwenye maduka yasiyosajiliwa aina 120 zenye thamani ya Sh. 20,067,100.

Aidha, Sillo amesema zoezi hilo litakuwa ni mwendelezo ambapo wataendelea kufanya kwa kushitukiza  kutokana  na uchunguzi ambao utakuwa ukifanyika katika maeneo husika.

Na kwamba, hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa ambapo jumla ya majadara 19 ya kesi yamefunguliwa katika vituo mbalimbali vya Polisi dhidi ya watuhumiwa hao.  Dar es Salaam kuna kesi 10, Arusha 2, Mwanza 1,na Mbeya 6

“Napenda kuwashukuru wale wote walioshiriki katika oparesheni hizi zikiwemo Taasisi za Baraza la famasi, Tamisemi, Bohari ya Dwa (MSD), Mamlaka ya Mapata Tanzania (TRA) na Taasisi ya Kupambana na kuzuia rushwa (TAKUKURU), ambao mlishirikiana na sisi katika zoezi hili naomba muendelee’. Amesema Sillo.

error: Content is protected !!