October 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TFDA yaipiga tafu Ilala

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Raymond Wigenje akimkabidhi madebe Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngirumi

Spread the love

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA), imeikabidhi Manispaa ya Ilala madebe 100 ya kuhifadhia takataka. Anaandika Faki Sosi, DSJ … (endelea).

Msaada huo umekabidhiwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Raymond Wigenje kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngirumi.

Wigenje amesema TFDA imejiwekea utaratibu wa kila mwaka kujali na kuthamini jamii kwa kushiriki katika kazi za jamii na kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo kutokana na kuwa TFDA ni sehemu ya Jamii.

“Tukiwa tunasherehekea miaka 12 ya TFDA tangu kuanzishwa, tumekuwa tukitekeleza jukumu la msingi la kulinda Afya ya jamii, tumejiunga na wananchi wa Dar es Salaam hususani Manispaa ya Ilala,” amesema Wigenje.

error: Content is protected !!