Monday , 5 June 2023
Home Habari Mchanganyiko TFDA yafunga machinjio Kongwa
Habari Mchanganyiko

TFDA yafunga machinjio Kongwa

Duka la nyama
Spread the love

MAMLAKA ya udhibiti chakula vipodozi na dawa TFDA imefungia machinjio ya ng’ombe ya Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kuendelea na huduma ya uchinjaji ng’ombe   kutokana na machinjio hizo kutokidhi vigezo vya mlaji, anaandika Dany Tibason.

Kaimu meneja TFDA kanda ya kati Dodoma Dk. Englebert Mbekenga ameeleza kupitia vyombo vya habari kuwa tangu Mei 12, mwaka huu mpaka watakapofanya marekebisho ndipo watafunguliwa kuendeleza huduma hiyo.

Mbekenga amesema kwa mujibu wa sheria namba (1) ya mwaka 2003 ya Chakula Dawa na Vipodozi imeweka wazi kwamba eneo linalohusika na uchinjaji mifugo ili liweze kutambulika kama machinjio inabidi liwe na maji ya kutosha kwa ajili ya kufanya usafi na vyoo vya kutoa huduma kwa wanyakazi wa machinjio.

“Lakini machinjio ya Kongwa haina huduma yoyote ya maji wala bomba na vyoo havina milango hali iliyopelekea utumiaji wa ovyo katika mazingira kwa baadhi ya watu kujisaidia ovyo na uchafu uliokithiri kutokana na ukosefu huo wa huduma ya maji,” Mbekenga alieleza.

Mmoja wa wamiliki wa bucha ambaye pia hutegemea machinjio hayo kwa masharti ya kutotajwa jina amesema kufungwa kwa machinjio hiyo kumeleta ugumu na kuongezeka kwa gharama kwani kwa inawalazimu kusafiri zaidi ya kilometa 16 kupata huduma katika machinjio ya Kijiji cha Mbande.

Ameiomba serikali kuchukua hatua mapema kufanya matengenezo kwani wao wamekuwa wakilipia kila kichwa kinachochinjwa kiasi cha 3,000/= na machinjio hutegemewa zaidi ya wafanyabiashara hao wa nyama.

Kwa upande wa bei ya nyama ya ng’ombe wilayani humo  kwa wauzaji waolikuwa wakiuza sh. 4,000/= kwa kilo kwa sasa wamepandisha mpaka 5,000/= kwa kilo.

Kadhalika Dk. Mbekenga ametoa wito kwa wamiliki machinjio binafsi na halmashauri zote kuhakikisha sheria, kanuni,na taratibu zinafuatwa na TFDA haitarajii kuona nyama safi inatoka katika machinjio zilizilizokithiri kwa uchafu.

Pia ametoa pongezi kwa vyombo vya habari kwa mchango wao mkubwa kwani kupitia habari wananchi watatambua mambo mbalimbali badala ya kubaki gizani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

Habari Mchanganyiko

Bandari ya Kigoma kuongezewa uwezo wa kutoa huduma zake

Spread the love  SERIKALI kupitia mamlaka ya Bandari nchini (TPA), imewekeza takribani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kifo cha mwanafunzi UDOM: Tume yamsafisha naibu waziri

Spread the loveTUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini (THBUB),...

error: Content is protected !!